Simba kuna vipaji havitumiki

Simba kuna vipaji havitumiki

Nilipoona DM watatu kwenye list nikajua tumekwisha.
Alivyo mpuuzi kocha wenu, no9 kaanza na Kibu D.
Nikamuuliza mbumbumbu alie karibu yangu, "unamuelewa kocha wako lakini?"........ Binafs hii mechi namlaumu kocha, kwanini hakuanza na namba 9 halisi?
Japo Jobe ni wakawaida lakini sio wakuwekwa nje na Kibu D.

Angeanza na Jobe wenda mungeambulia hata sare.

Yote kwa yote nawashukuru Ali Ali kwa kunikamatia kenge, maana alishaanza kuleta mazoea.
 
Simba inatatizo la kutokuwa na viungo wanaodrive mipira na kupunguza watu, na umaliziaji pia. Tunataka wachezaji wa viungo wanaotembea na mpira kama iniesta, xavi, modrick, Sasa mchezaji akipata mpira pasi tu Hasogei hata Hatua nne
Kama yule Sarr yaani ana pasi za kusakizia na papatu nyingi yaani akipewa pasi unaogopa maana muda wowote anaweza pokonywa.
 
Yap matokeo yake mtu akipata mpira ni pasi tu kutembea hawezi mfano babacar sarr walau ngoma lakini na ye bado labda inatokana na waliomzunguka

Simba ambayo kwangu Mimi ni best ile iliyotolewa na kaizer chiefs tulikua na viungo wanaotembea na mpira kupunguza watu ikibidi hata mashuti ya mbali ikibidi
Yaani yule Sarr sijawahi muelewa kwanza hajiamini akifanyiwa press atapiga pasi ya kusakazia au atarudisha nyuma.
 
sometimes hua nashindwa kuelewa kocha benchika malengo ya kuanza na viungo 3 wakabaji kiasili ngoma,kanoute na babacar halafu mbele kuna playmaker 2 na straika 1.

Naamini/naona kuna wingers ambao wana uwezo lakini hawapewi nafasi mfano miqquesone na chasambi ukiangalia hao viungo wote sio creativity iwapo mkiwa mnacheza na timu inayozuia kama Al Ahly.

Unapocheza na timu inayopaki basi at least uwe na wachezaji wanyumbulifu wenye kasi ambao wanaweza fungua timu mfano miqquesone na chasambi halafu ukabaki na na ngoma akasimama nyuma.

Naamini kabisa simba inatakiwa ianze kutumia mawinga halisia ili walau kutengeneza connection kutoka kiungo cha juu na cha chini huku ikipunguza viungo wakabaji na saidoo atolewe kabisa.

Mwishoni timu nzima ilionekana kuchoka inonga sijui kalala wapi Leo,kibu kapambana na timu imecheza lakini ndo hivo matokeo hayaji hivi hivi lazima kuwe na mipango na wachezaji wenye creativity in case mipango imefeli ambao hawatumiki Miqquesone/ Chasambi.

NB;Ahmed ally si muda atakosa mvuto watu wanahamasika kuisupport timu kulingana na matokeo na si propaganda mpira ni mchezo wa wazi kila mtu anaona
Wote wazee hao.
 
Onana ni hopeless player, ni ajabu eti Phiri aliondoka.
Onana ni mchezaji wa hovyo kabisa akikupa matokeo mechi 1 utasubiri mechi nyingine 10 akupe tena performance nzuri anacheza kibishoo
Akipoteza mpira hakabi yani tafrani tupu

Walau miqquesone anakupa kitu mapinduzi cup alikua kasharejesha kiwango chake tumerudi ligi kuu kaanza kupigwa tena benchi..

KAZI IPO KWAKWELI
 
Yap matokeo yake mtu akipata mpira ni pasi tu kutembea hawezi mfano babacar sarr walau ngoma lakini na ye bado labda inatokana na waliomzunguka

Simba ambayo kwangu Mimi ni best ile iliyotolewa na kaizer chiefs tulikua na viungo wanaotembea na mpira kupunguza watu ikibidi hata mashuti ya mbali ikibidi
Viungo walikua nani na nani?
 
Phiri alikuwa na ugomvi na viongozi asingewez kuchepa pale msimbaz bora alivyoondoka
Alikataa kuwapa 10% ..hio ndio shida iliyopo, siku watakapotoka huyo try again na baadhi ya wanachama na kuzuia mianya ya utapeli na uwakala simba ndio atakua bingwa CAF, na huku ligi.kuu ndio tusahau kabisa...miaka 5 yanga atakua bingwa. Hapo akili ndio zitakaa vizur
 
Alikataa kuwapa 10% ..hio ndio shida iliyopo, siku watakapotoka huyo try again na baadhi ya wanachama na kuzuia mianya ya utapeli na uwakala simba ndio atakua bingwa CAF, na huku ligi.kuu ndio tusahau kabisa...miaka 5 yanga atakua bingwa. Hapo akili ndio zitakaa vizur
Barbra alijitahidi sana kuwafinya walafi pale msimbazi ila unajua waswahili wanapenda majungu wakayapika haswa ilibidi mwanadada ake pembeni
 
Back
Top Bottom