Simba kupata bao kwa Nkana sio shida, shida ni kuwazuia nao kupata bao

Mchezo wa club bingwa Africa utakaopigwa leo uwanja mkuu wa taifa leo kati ya Simba na Nkana red devils ya pale kitwe Zambia,dhahiri shahili inaonyesha Nkana wananafasi kubwa ya kupata matokeo ugenini huku wakiwa wanaongoza goli 2-1.Huku simba wakihitaji goli moja tu ili kufuzu lakini mashabiki wengi wanawasiwasi na pazia lao pale langoni kama linaweza kuhimili dakika 90 bila kuruhusu huku wakiwa nabeki mbovu kabisa ya wawa ambaye hana speed na umri umenoga,japo wengi wanalialia aanze juko ambaye yeye dakika kumi nyingi atakuwa kala umeme(red card) kwa namna anavyocheza kama mieleka.

Mashabiki wa Simba jiandaeni kisaikologia kwa matokeo ya leo pale Taifa au hata mkienda kucheza sebuleni kwa Mo bado matumaini ni sifuri.

Kila la heri MTANZANIA mwenzetu Hassan Kessy ktk mchezo wa leoView attachment 975185
...... Wewe mwandishi na mawazo yako finyu, yasioona mbali dua lako mbaya Kwa Simba likurudie wewe na Yanga yako
 
Iko siku tutapigana vita Halafu tukaombwa support Na adui tukatoa jinsi tulivo nyumbu
Mungu ubariki Simba
Mungu bariki Tz

#Kufanakupona
 
Mchezo wa club bingwa Africa utakaopigwa leo uwanja mkuu wa taifa leo kati ya Simba na Nkana red devils ya pale kitwe Zambia,dhahiri shahili inaonyesha Nkana wananafasi kubwa ya kupata matokeo ugenini huku wakiwa wanaongoza goli 2-1.Huku simba wakihitaji goli moja tu ili kufuzu lakini mashabiki wengi wanawasiwasi na pazia lao pale langoni kama linaweza kuhimili dakika 90 bila kuruhusu huku wakiwa nabeki mbovu kabisa ya wawa ambaye hana speed na umri umenoga,japo wengi wanalialia aanze juko ambaye yeye dakika kumi nyingi atakuwa kala umeme(red card) kwa namna anavyocheza kama mieleka.

Mashabiki wa Simba jiandaeni kisaikologia kwa matokeo ya leo pale Taifa au hata mkienda kucheza sebuleni kwa Mo bado matumaini ni sifuri.

Kila la heri MTANZANIA mwenzetu Hassan Kessy ktk mchezo wa leoView attachment 975185
Leo mtaukimbia huu uzi. Nkana anakula 4-1.
 
Wanasimba na Watanzania wazalendo,

Kesho Simba inawakilisha nchi kwenye mechi muhimu kabisa ya marudio. Kikosi cha sasa cha Simba inawezekana kuwa moja ya vikosi bora kabisa toka club hii ianzishwe labda ukitoa vikosi vichache kikiwemo kile kilichofika fainali kombe la CAF mwaka 93.

Ninaomba technical coach wa Simba amtumie stopa tegemeo wa Uganda Cranes Juuko Murshid kama beki wa kati akisaidiwa na Wawa huku Erasto Nyoni akicheza kama beki wa kulia.

Vile vile asiwatumie John Boko na Kagere kwa pamoja bali ni vema mmoja aanze ili timu iwe na wachezaji wengi wenye uwezo wa kuwapikia wafungaji.

Kocha ndiye mwenye maamuzi na ufahamu wa kutosha kuhusu wachezaji na mfumo anaotaka lakini na sisi mashabiki si mbaya tukiwashauri kwa jicho letu la jukwaani.

Kila lakheri mnyamaaaaa!
Pale nyuma mikia ni majanga tu hakuna afadhali wote ni chujio tu
 
...... Wewe mwandishi na mawazo yako finyu, yasioona mbali dua lako mbaya Kwa Simba likurudie wewe na Yanga yako
Vyura wanatamani kuona Simba ikifungwa ili wapate furaha na kwa hakika leo watakuwa kwenye hali mbaya sana

Simba nguvu moja
 
Back
Top Bottom