Simba kusajili Beki ni kweli ndio uhitaji wa Simba kwa sasa?

Simba kusajili Beki ni kweli ndio uhitaji wa Simba kwa sasa?

Mtoto wa nzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
10,017
Reaction score
18,537
Kwanza niweke kumbukumbu sawa mimi ni shabiki wa Yanga... Pili kwa Simba ya msimu uliopita ilikuwa ya kuongeza wachezaji wachache tu kiungo wa juu mmoja wa chini mmoja kipa na striker wawili wa kutumainiwa, kwenye striker wamefanya vizuri wamemrudisha Okwi lakini tunaona asipokuwepo timu inapata shida sana kufunga japo inatengeneza nafasi nyingi sana, sehemu ya kiungo inafanya majukumu yao sahihi pasi na shaka, ukija ulinzi Nyoni, Mwanjali, Mlipili, Mbonde, Tshabalala, Ally Shomari Hata na Kotei wanaitendea haki....

Bado ule upungufu wao wa msimu uliopita umebaki kwenye nafasi ya ushambuliaji lakini bado wanasuasua kupafanyia kazi. Leo wamesajili Beki kutoka Ghana Maliki Ismaila na wanamuacha Mavugo sawa Mavugo ili huyu apate nafasi sawa Mavugo hajafikia malengo ya timu, kwa nini usitoe Mavugo ukaleta Chuma kikali cha ushambuliaji!!??

Nasikia Kuna mfungaji bora wa Rayon Sport anakuja hiyo maana yake Kuna mchezaji mwingine wa kimataifa atakatwa...

Unamsajili mchezaji wa kimataifa kwa gharama anakuja anakaaa benchi kama ilivyokuwa kwa Blagnon na sasa Gyan afu katikati ya msimu tunamuacha. Si Ni kuchezea pesa huku.

Na hii iwaendee na Yanga pia japo wanacheza lakini hawafikii yale tunayotarajia ni heri hizo pesa tukawaboreshea maslahi wachezaji wetu wa ndani kuliko kupiga pata potea za kindezi kama Juma Mba na kina Niang mzee wa Powerbank.
 
hahahaha ivi pape ndaw yu wapi?

simba wakati mwingine huwa wana mambo ya ajabu sana
 
Dah nikimkumbuka Papa Ndaw nacheka sana aisee,wakina Kaburu na Pope sio watu kabisa mmamaeee.
 
Simba wanahitaji washambuliaji wakali tu.
Kila idara imetimia isipokuwa ya ushambuliaji.
 
ningekuwa dar ningeenda makao makuu ya simba kuwachapa viboko viongozi wa simba wanashindwa kumleta mshambuliaji wanaleta beki,simba hatuna tatizo na beki
 
okwi nae ni kma ali bahatisha game ya Ruvu shooting
 
Anaondoka Mwanjali thats why unamuona Asante kuna walakini pia kwa Juuko
 
Anaondoka Mwanjali thats why unamuona Asante kuna walakini pia kwa Juuko
Mwanjali ni mzuri ila umri umeenda Juuko ni mzuri aachwe hapo wakutemwa ni Mavugo, Gyan, na Manjali kwa professionals locals kapombe. Mwambeleko. Kazimoto.
 
Omba nafasi ya ushauri kwenye kamati ya usajili ya Simba usituchoshe hapa
 
Mleta uzi umegusa penyewe. Yaani hii kamati ya usajili chini ya Hanspope huwa siielewi kabisa. Ikihitajika beki wanaleta mshambuliaji. Ikihitajika mshambuliaji wao wanasajili beki. Simba ya sasa imetulia kuanzia nyuma mpaka katikati.

Hata winga zipo vizuri sana. Shida ipo kwa washambuliaji. Wanatakiwa wasajili washambuliaji wa kati wawili tu basi ili kumpa changamoto Boko. Halafu timua Mavugo, Luizio, Gyan mishahara yao ongezea kina Kichuya, Mzamiru, Nyoni n.K.

Lakini cha ajabu utasikia mshahara wa Mavugo ni mara nne ya Kichuya. Haya ndio maajabu ya kamati ya Hanspope. Halafu kichuya akisema anaondoka kama alivyofanya ajib utasikia huyu kichuya sio mzalendo acha aende.

Hivi inahitajika hesabu gani kuona kuwa kazi anayofanya kichuya uwanjani ni mara kumi zaidi ya mavugo? Namuomba mo akichukua timu kitu cha kwanza aivunjilie mbali hii kamati ya usajili aweke watu wanaoujua mpira kama kina Mwameja, Mogela , Mtemi Ramadhani, Malota soma n.k.
 
Back
Top Bottom