Simba kuweni makini na Senzo

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Huyu jamaa kwa jinsi alovyoondoka ni dhahiri yuko kwenye vita vikali sana na Simba vikiendeshwa chini chini.

Hata msishangae sana kile kipigo south Africa alihusika katika kutengeneza fitna.

Sasa kwenye hii kesi ya Morrison,naamini ana nyaraka za siri na zinaweza hata kuwa za kughushi,kwani alikuwa na mamlaka makubwa pale Simba.Nani ajuaye kama nyaraka hizi hazitatumika kuwahukumu Simba?
Je ana mawasiliano gani na rais wa CAF?

Simba msimchukulie poa huyu jamaa,kwani anafuatilia nyendo zenu zote na siku mkikosea tu na kuingia kwenye 18 zake,mmekwisha.

Huyu jamaa ameamua kuufanya utani wa Simba na Yanga kuwa ugomvi wa kimataifa unaofanywa kimafia.Hawa wa south wana roho mbaya sana na vidasi vyao haviishi.Msije mkashangaa mnashushwa daraja. Muda utaongea
 
Kwani wao wanasemaje huko.
Naona mmeshikwa penyewe huko haswaaa
 
Usitutoe kwenye reli...... Sisi tumefocus kwenye kushinda mechi zetu tupate ubingwa.
 
Ata akiungana na ndugu zake wote wa huko ,South Africa hawezi kuifanya chochote Simba
 
Hakuna kesi ya Morrison popote, hao watangazaji njaa wa michezo huwa wanatumiwa na mabwana zao kuiharibia Simba bila sababu nimeshawazoea.
 
Sawa naweza kuwa mjinga.Lakini jiulize alipataje ujasiri wa kujaribu kuingilia mechi kati ya Tanzania Prisons na Simba tena nje ya Dar?Kama ni mgeni kweli mbona alifanikiwa katika mpango wake?
Haya we mwenyeji mjanja ulikuwa wapi kuzuia mikakati ile?
We mjinga sana unaogopa mgeni ukiwa nchinii kwako.yule tunamtafutia kesi ya unga tu tunafukuza nchini
 
Hana lolote na ajue yeye ni mgeni tu hapa anaweza kufanywa lolote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…