Simba kuzuiwa kufanya mazoezi, Je inamfanya kutofika uwanja kucheza mechi? Kanuni ya 31.

Mbogi

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2021
Posts
803
Reaction score
997
Baada ya Mashabiki wengi wa soka kuumizwa na usitishwaji wa derby wamekuwa wakitaka kujua, Je hata kama simba angekuwa alikosewa kikanuni, tukio hilo linampa fursa ya kugomea mchezo! JIBU NI NDIYO.

Kanuni ya 31 ya Tff/tplb inasomeka hivi;
"Timu yoyote itakayo kosa kufika uwanjani bila ya sababu za msingi zinazokubalika ktk kanuni za TFF/TPLB na / au kusababisha mchezo usifanyike itakabiliwa na adhabu zifuatazo" (zimeainishwa sita)

Kumbe kanuni hii inakubaliana na uwepo wa sababu ya msingi inayokubalika kwa tff/tplb inayoweza kuifanya timu isifike uwanjani. Ieleweke kuwa sababu hiyo iwe ni sehemu ya uvunjifu wa kanuni.

Hivyo basi Simba wanayo sababu ya msingi inayokubalika ktk kanuni za Tff/Tplb ya uvunjifu wa kanuni ya 17(45) iliyofanywa na ama wahusika wa uwanja au wapinzani wa Simba.

Na ikumbukwe kuwa sababu kama hii pia ndiyo iliyo sababisha timu mgeni Nigeria kutofika uwanjani Libya baada ya kufanyiwa vitendo vya kihuni, (kutelekezwa uwanja wa ndege kwa masaa 12) na uamuzi wa CAF ukaamua kuwa Nigeria walikuwa na sababu na hivyo wakapewa alama 3 na goli 3 dhidi ya Libya.

Kabla ya hukumu, vyanzo vya tukio huzingatiwa kwa umuhimu mkubwa. Karibuni kwa hoja.
 
Baada ya Mashabiki wengi wa soka kuumizwa na usitishwaji wa derby wamekuwa wakitaka kujua kuwa hata kama simba alikosewa kanuni inampa fursa ya kugomea mchezo! JIBU NI NDIYO.

Kanuni ya 31 ya Tff/tplb inasomeka hivi;
"Timu yoyote itakayo kosa kufika uwanjani bila ya sababu za msingi zinazokubaka kwa TFF/TPLB na / au kusababisha mchezo usifanyike itakabiliwa na adhabu zifuatazo"

Kumbe kanuni hii inakubaliana na uwepo wa sababu ya msingi inayokubalika kwa tff/tplb inayoweza kuifanya timu isifike uwanjani. Ieleweke kuwa kuwa sababu hiyo iwe ni sehemu ya uvunjifu wa kanuni.

Hivyo basi Simba wanayo sababu ya msingi inayokubalika ktk kanuni za Tff/Tplb ya uvunjifu wa kanuni ya 17(45). Na ikumbukwe kuwa sababu hii pia ndiyo iliyo sababisha timu mgeni Nigeria kutofika uwanjani Libya baada ya kufanyiwa vitendo vya kihuni, (kutelekezwa) uwanja wa ndege kwa masaa 12) na uamuzi wa CAF ukaamua kuwa Nigeria walikuwa na sababu na hivyo wakapewa alama alama 3 na goli 3.

Kabla ya hukumu vyanzo vya tukio huzingatiwa sana. Karibuni kwa hoja.
Kupata VITUKO kama hivi andika
Tff KWENDA no 15777
 
mbogi kama mbogi...
 
Back
Top Bottom