Na ule uwanja wetu wa Kaunda kwa nini tusijenge mabwawa ya samaki kwa ajili ya kuwauzia majirani na pia kuwagawia wachezaji wetu kama sehemu ya motisha pale wanapofanya vuzuri kwenye mechi zao?
Maana Yanga na simba baba yao ni mmoja!! Tangu miaka ya 1930's! Mpaka leo wanategemea viwanja vya serikali. Yaani timu zilizoanzishwa miaka ya 1990's na 2000's kama Azam Fc, Mtibwa Sugar, Ihefu Fc, Namungo Fc, nk zina viwanja vyao!
Ila ukija kwa Yanga na simba, kila siku viongozi wao wanapiga tu porojo, na kuwahadaa mashabiki na wanachama.