Kwa bahati nzuri navyowajua mashabiki wa Simba kwa mpira ni kama sharehe fulani tu ambayo hata ikiwaletea maumivu basi ni siku 2 ama 3 tu maumivu yanapoa, na hata ile maumivu huwa sio kivileee.
Jamani huku Yanga hali ni mbaya sana, Wananchi huwa mood zinavurugika vibaya mno, mbovu, mbaya. Yanga hii kwa wengi ni kama mwanafamilia, yaani ikishuka ama ikizingua yaani sijui hata nisemaje, hata mwezi mtu anaweza kukaa anasononeka japo mnamuona ni mwenye furaha ila mkigusia tu Yanga anakuwa mnyonge.
Hata viwanjani huwa kunakauka kwa matokeo yanayowaumiza mashabiki, hata wakienda na wakaonekana ni wengi bado ni wachache sana kwenye kundi la Wananchi ambao wapo tayari kwenda viwanjani.