Habari za ndani kabisa tulizozipokea zinaeleza ya kuwa mojawapo kati ya hizi klabu mbili kongwe hapa nchini ipo mbioni kupigwa mnada.
Japo chanzo chetu cha kuaminika hakijaitaja moja kwa moja klabu hiyo, ila wadau mbalimbali wa michezo wameihusisha timu ya Simba kuwa ndio mlengwa kutokana na ukata mkubwa unaoikabili hapo klabuni hali iliyopelekea wachezaji kushindwa kulipwa mishahara na posho, kushindwa kuajiri kocha mkuu pamoja na timu kukosa usafiri wa basi.
Pia ukata mkubwa uliyoikumba klabu iyo umepelekea kushindwa kutenga bajeti ya usajili dilisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.
Taarifa zaidi zinadokeza ya kuwa Mwekezaji wa klabu iyo ameikacha klabu hiyo huku mtendaji mkuu wa klabu nae akiandika barua ya kujiuzulu wakati ambao mwenendo wa timu kwenye ligi ukiwa ni wakusuasua.
Wadau mbalimbali wameiomba serikali iingilie kati ili kuinusuru klabu hii kongwe isije kupotea kwenye ramani ya soka la nchi hii kama ndugu zao African Lyon FC walivyopotea