Simba mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu

Simba mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu

mtimbange

Senior Member
Joined
Jan 21, 2015
Posts
104
Reaction score
32
Juz TAMBWE kafanyiwa vbaya na wale mijida Simba wakasema yanga wagangamae,leo viongoz wa simba hao hao wanaitaka TFF imchukulie hatua Aggrey Morris kwa kumpga kiwiko Okwi,wamesahau matusi yao kwa yale alofanyiwa TAMBWE kwel mkuki kwa nguruwe
 
Mpira wa Bongo, ushabiki hata kwa yasiyofaa kushabikiwa!!
 
Na kati ya hayo mawili (Tambwe na Okwi) lipi la kimpira na lipi la makusudi?
 
Yote sio ya kimpira. Marefa njaa na dhaifu wanatuharibia ligi,bila kusahau ulegelege wa TFF.
 
Na kati ya hayo mawili (Tambwe na Okwi) lipi la kimpira na lipi la makusudi?
Mkuu faulo zote uwanjani zinazohusisha mikono ni faulo za kukusudia na sio za kimpira, nimeona video na kiwiko cha Aggrey kwenda kwa Okwi hicho ni cha makusudi kabisa na hilo halina ubishi. Picha zilizoonekana za Tambwe na George nazo nyingi zimehusisha mikono hivyo ni kukusudia na kuamua kumtoa mtu mchezoni kwa njia za kipuuzi.

Huwa nashuhudia kadi nyekundu zinatolewa kwa mchezaji anayempiga mwenzake kiwiko hata kama wote wameruka juu na wanawania mpira lakini endapo mmoja atatumia kiwiko kadi nyekundu inamhusu.

Kwa Okwi inaonekana wote wawili hakuna aliyekuwa na mpira na Okwi alikuwa kasi akijaribu kutafuta nafasi ili apigiwe pasi badala yake Aggrey akamtuliza kwa kiwiko (bahati mbaya hakuadhibiwa, huenda refa hakuona au aliamua kupuuzia) na refa naye hajaadhibiwa labda ataadhibiwa baadaye angalau ishu ya Tambwe refa ameadhibiwa.
 
Back
Top Bottom