Simba mmesharekebisha eneo la namba 10?

Singasinga

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2011
Posts
2,711
Reaction score
3,279
Habari wakuu

Nadhani wote tumeshuhudia kwa hizi game team ilizocheza imefia kwenye namba 10. Nafasi za kufunga hazitengenezwi kabisa.

Kuelekea game za CAF je Hilo tatizo limeshapata mwarobaini?

Nawasilisha.
 
Inategemea na benchi la ufundi. Je benchi la ufundi linajua tatizo la timu yao kukosa matokeo chanya ni hiyo nafasi ya namba 10? Au inawezekana benchi la ufundi lenyewe kwa utaalamu wake linajua kitu tofauti na hiyo namba 10 kuwa ndio inasababisha isipate matokeo chanya.

Tusubiri tuone jumapili kama wamefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika michezo uiliyopita kwani usiku wa deni haukawii kukucha.
 
Ngoja tutaona kwenye game za ushindani zinazofatia.walimu lazima wabadili mbinu Chama na Merquisone hawapo tena waliopo ni wengine sio wenye cariba kama ya wale.
 
Mpira ni mchezo wa wazi na hata sisi tusio makocha tunaweza ona ombwe lilipo
Simba imefia namba10,Bwalya kashindwa kubeba majukumu ya mtangulizi wake ingawa bench la ufundi na mashabiki tuliweka tumaini kwake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…