Simba mrejesheni dimbani Jonas Mkude

Mimi ni shabiki kindakindaki wa Simba binafsi toka huyu jamaa awe nje ya uwanja pengo lake linaoneka na hata baada ya kusajili Thadey Lwanga. Namshauri kocha wangu wa simba amrejeshe dimbani shujaa wetu jonas mwana mkude.

Naomba kuwasilisha
Mwanayanga mwenzangu lini umehamia Simba? Ninyi mnakuwa vigeu geu hamna mapenzi ya dhati kwa Yanga
 
Mimi ni shabiki kindakindaki wa Simba binafsi toka huyu jamaa awe nje ya uwanja pengo lake linaoneka na hata baada ya kusajili Thadey Lwanga. Namshauri kocha wangu wa simba amrejeshe dimbani shujaa wetu jonas mwana mkude.

Naomba kuwasilisha
Nidhamu kwenye kazi yako ni jambo la kwanza kabisaa ili kuendelea kufanya vizuri.
Wachezaji wa kibongo ni bangi zinawaharbu..ila kwa sasa watajifunza tuu kuwa na nidhamu..mana wachezaji wa nje wanareplace nafasi zao..
 
Ni kweli wamrudishe fundi , kwa kipindi alichotumikia adhabu atakuwa ameshajirekebisha!
 
Hizi match za nyumbani wanaweza mpanga mkude
Lwanga aingie kipindi cha pili mwishoni
A reserve energy ya sudani.
Asije Umia tena
Uko sahihi, za nyumbani atacheza nyingi tu, Lwanga na baadhi ya wachezaji inabidi kocha awalinde sana towards mechi za kimataifa.
Ila ikija tokea akaanza na Lwanga mechi yoyote ile, Mzamiru nafasi yake itakua matatani kwenye machaguo ya kocha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…