Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wee umeanza kushangalia simbaa hii ya kina bocco kijanaa haya maji ni marefu kwako kaa kimya uufiche ujinga wakoUna harufu ya utopolo, lengo lako ni kuchonganisha na kuleta taharuki, lakini umeshindwa!! Uto huwezi kutupangia timu!! Wachezaji wote ni wa Simba na yeyote anaweza kupangwa na kocha!!
Kumbe kwenye mpira pia uponaona amepangwa, yupo kwenye kikosi kinachoanza leo
Ndiyo maana Nakuelewa sana basi tu nina nyoto ya pundandiyo nipo kiasi[emoji3]
Anawapiga wenzake misumari sasa kwa Mganda kafeliMkude ajilaumu mwenyewe. Alichezea kazi yake kwa kuleta nyodo muda mrefu sana viongozi wakamletea Kotei wapambane akammudu. Akaletwa Fraga akapata majeraha. Sasa hapo kwa mwamba Lwanga viongozi ndio wamemkata nyodo zote kabakia na watetezi wachache mitandaoni. Vile vitisho vyake kila wakati eti anaenda Yanga avilete sasa hivi tena kama viongozi hawatampeleka Yanga bure kabisa. Na mbaya zaidi Fraga anaendelea vizuri na matibabu huko Brazil huku Doxa Djikanji yupo hapo Kongo anapiga jaramba na anataka namba dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa juni/julai mwaka huu. Muzamiru naye gari limeshawaka na mapafu nyake ya mbwa akijirekebisha tu kidogo kwenye kutoa pasi basi Mkude atakuwa na hali ngumu zaidi. Na hivi Mkude hajacheza muda mrefu itamchukua muda kiasi kurudisha kujiamini kwake kama mwanzo. Na mchezaji anajenga kujiamini pale anapocheza mara kwa mara kitu ambacho ni kigumu sana sasa hivi kucheza mara kwa mara kwa timu yenye kikosi kipana kama Simba.
Yote kwa yote Mkude alikuwa na mapungufu makubwa ; kukaba kwa macho, "square pass"" kwa mabeki wake wa pembeni muda wote wa mchezo badala ya kupeleka mpira mbele kwa haraka, faulo za kijinga akizidiwa, kuangalia chini muda mwingi anapokuwa na mpira badala ya kuinua macho ili apige pasi za mbali, kushindwa kucheza mipira ya 50/50 na viungo wa timu pinzani (hafiki maungoni kama anavyofika mwenzake Lwanga) na uwezo mdogo wa kunusa hatari pindi Simba inaposhambuliwa. Sasa hivi Wawa na Onyango wanaonekana uwezo wao halisi baada ya kuwa Lwanga anawalinda jinsi inavyotakiwa. Lakini kipindi Wawa na Onyango wakicheza na Mkude kila mtu alimuona Wawa kaisha na kazeeka. Lakini Mwangalie Wawa wa sasa hivi chini ya Lwanga kwenye mechi za As Vita na Alhaly utaona tofauti kubwa sana na Onyango ndio kawa bora kabisa. Makosa ya Mkude yalikuwa hayonekani kwa urahisi kwa sababu alikuwa anafanyia katikati ya uwanja matokeo yake lawama zilikuwa zinaenda kwa watu wa mwisho Wawa na Onyango.
Kwa nidhamu yake mbaya iliyopitiliza ilifika mahali mpaka wachezaji wenzake walimgomea asirejee kambini kwani atawavuruga. Kwa hali hiyo Mkude inabidi abadilishe mienendo yake nje na ndani ya uwanja vinginevyo inaweza kuwa ndio mwisho wa kucheza timu kubwa kwani sasa hivi hata akienda Yanga atakutana na mafundi Fei Toto na Mukoko kwa hiyo itabidi asubiri benchi kwanza mpaka mmoja wao aumie au awe na kadi.
Kwa ufupi Mkude amejipa kazi kubwa sana ambayo itambidi apambane hasa ili kurudi kwenye "first eleven"" na ni lazima akubali kubadilika na kujifunza kwa Lwanga namna ya kukaba na kikubwa zaidi ajifunze nidhamu kwa sababu nidhamu ndio mwanzo wa mafanikio yoyote yale mahali popote pale.
Unyambulifu unaisadia nini timu kama mkude huwa hawezi kukaba mpaka awekewe mtu wa kukabaShida yangu ni ombwe kubwa (gap) lililopo kati ya kiungo mnyambulifu jonas mkude na lwanga
Kumbe ndio maana wenzake walimgomea kurudi, dah mbaya sana.Anawapiga wenzake misumari sasa kwa Mganda kafeli