Inavyoelekea huko majuu hali imemuwia ugumu. Mpaka sasa zimechezwa mechi zaidi ya kumi na Okwi amejumuishwa mara mbili tu kikosini. Mara ya kwanza aliingilia kama mchezaji wa akiba akicheza kwa dakika tatu tu. Mara ya pili alijumuishwa kama mchezaji wa akiba asiingie kabisa uwanjani. Tangu hapo hata benchi hakai. Naomba sisi wadau wa mikia tuwashinikize uongozi wamrejeshe kundini ili aifunge Yanga.