Simba msikurupuke Victorien Adebayor ameshuka kiwango

Simba msikurupuke Victorien Adebayor ameshuka kiwango

Salaam,

Viongozi wa Simba nawapa tahadhari tena msije kukurupuka kumsajili Victorien Adebayor raia wa Niger aliyeshuka kiwango sana

Mchezaji huyu amepoteza namba kwenye taifa dogo kimpira Niger
Ni miaka miwili yuko bench kutokana na kushuka kiwango toka alipohamia RS Berkane hawajawahi kucheza hata mchezo wa kirafiki

Na sasa yuko Amazulu akisuburia benchi na team ya Amazulu ina mpango wa kumwacha kama free agent

Za ndani ni kwamba week iliyopita alifika Dar es Salaam kusaini Simba
Simba wanaendelea kukurupuka kwenye usajili kama kawaida yao na wakipigwa 5G wataanza kulalama ati wachezaji wamerogwa

Scouting team ya Simba imelala hadi wameamua kusajili hili garasa Adebayor

5G itawakuta tena miaka 10 mfululizo hadi viongozi wenu watakapo pata akili
 
Viongozi wa Simba ndiyo sajili wanazopenda ,mchezaji akiwa kwenye kiwango hawana Hela(ubahili)ila akishuka kiwango ndiyo wananyemelea kama fisi.
Kiufundi huyo adebayo na Manzoki Kwa kusajiliwa Simba itakuwa mwendelezo wa dharau Kwa mashabiki.
Dawa ni kuisusia Simba kwenye michezo yote washangilie hao Viongozi.
 
Simba viongozi wana matatizo, wanataka adebayor(winger wa kushoto) je simba ina shida ya winger,? Je mido haina shida, je wasaidizi wa kapombe na tshabalala wapo?
Chama langu siku hizi limekuwa la hovyo sana, mijitu iliyopo pale huenda haijui soka, ni mijitu ya kukurupuka.
Wanayoyafanya pale ni kama wanasiasa wa bongo tu, kupanda gari la milioni mia 4 ila akifika kwenu anapanda punda mjione mko nae sawa. 😂🤣

Yaani Simba wanasikitisha Sana wanapenda dezo kuliko mala mala malaya wa uwanja wa fisi? Yote hii ni Mangungu
 
Ndiyo kawaida Yao Simba kufanya sajili za hivyo we fatilia ni wachezaji wachache sana ndiyo unakuta wapo kwenye ubora Kwa wakati huo wanasajiiwa Simba ila wengi wanaobaki ni wastaafu ,wamechoka huko walikotoka wakifika Simba tunaamishishwa ndiyo sajili za fainali.
 
Back
Top Bottom