Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kuna ajenda gani kati ya Rais Samia na Vilabu vya Simba na Yanga?, Wanatumika kisiasa na kufanya kampeni kabla ya wakati
Kuna namna CCM wanawatumia hawa wasemaji wa vilabu hivi pendwa nchini kujinufaisha kisiasa kipindi hiki kuelekea Uchaguzi, badala ya kuwekeza nguvu kwenye miradi ya maendeleo na kugusa maisha ya watu wa chini wakidhani labda kutumia watu wenye nguvu ya ushawishi ndio kujizolea mashabiki wao, siku hizi mambo yamebadilika, watu wanauelewa kwani kinachotakiwa ni kubadili maisha moja kwa moja ya wananchi.
Sasa hivi vilabu hivi vimekubali kubeba ajenda za kisiasa hadi kufikia hatua wana print picha ya Rais Samia kwenye T-Shirt zao zikiwa na maneno eti “Watoto wa Mama”, haya mambo sidhani kama yana impact zaidi ya kuleta mpasuko tu wa mashabiki. Kiongozi kama ni mtendaji mzuri haina haja ya mbwembwe hizi ili kupata watu au kura.
Pia, Soma:
+ Simba na Yanga hutumika kuzima vuguvugu au kusahaulisha wananchi changamoto zao za kijamii