Simba na Yanga acheni kutumika vibaya, kuibeba CCM, sasa hii "Watoto wa Mama" ya nini?

Sheria za FIFA zinakataza kufanya siasa kwenye michezo.
Mimi binafsi sipotezi muda wangu kwenye kushabikia mpira wa Tanzania na Africa.
 
Shida ilianzia hapo ndio maana kila mmoja anaona alidai uhuru kutoka kwa mabeberu
Hahaha.................hapo hapo tunaambiwa Vyama vya TAA na ASP baadaye TANU ndivyo vilivyodai Uhuru.

Huku tena tunaambiwa Vilabu vya Simba na Yanga vilitumika kudai Uhuru

Baadaye tena wanajitokeza Wazee wa DSM wakisema wao ndiyo walidai Uhuru 🙌
 
Kuna ajenda gani kati ya Rais Samia na Vilabu vya Simba na Yanga?, Wanatumika kisiasa na kufanya kampeni kabla ya wakati

Kuna namna CCM wanawatumia hawa wasemaji wa vilabu hivi pendwa nchini kujinufaisha kisiasa kipindi hiki kuelekea Uchaguzi, badala ya kuwekeza nguvu kwenye miradi ya maendeleo na kugusa maisha ya watu wa chini wakidhani labda kutumia watu wenye nguvu ya ushawishi ndio kujizolea mashabiki wao, siku hizi mambo yamebadilika, watu wanauelewa kwani kinachotakiwa ni kubadili maisha moja kwa moja ya wananchi.

Sasa hivi vilabu hivi vimekubali kubeba ajenda za kisiasa hadi kufikia hatua wana print picha ya Rais Samia kwenye T-Shirt zao zikiwa na maneno eti “Watoto wa Mama”, haya mambo sidhani kama yana impact zaidi ya kuleta mpasuko tu wa mashabiki. Kiongozi kama ni mtendaji mzuri haina haja ya mbwembwe hizi ili kupata watu au kura.
Pia, Soma:
+
Simba na Yanga hutumika kuzima vuguvugu au kusahaulisha wananchi changamoto zao za kijamii
Mmezuiwa kuzitumia?
Kulalama ndio mnachoweza
 
Wapeleke hizo hela huko vijijini wakawaboreshee maisha, huko ndiko wana wapiga kura kuliko kufanya hivi
Hizo ni personal issues wala haihusiani na club kama na wewe unahitaji kufanya hivyo endelea tu ni mapenzi yako bwana.
 
Hahaha.................hapo hapo tunaambiwa Vyama vya TAA na ASP baadaye TANU ndivyo vilivyodai Uhuru.

Huku tena tunaambiwa Vilabu vya Simba na Yanga vilitumika kudai Uhuru

Baadaye tena wanajitokeza Wazee wa DSM wakisema wao ndiyo walidai Uhuru 🙌
😂😂 tutafika tumechoka sana
 
UKISHABIKIA SANA SIMBA NA YANGA AUTOMATICALY AKILI ZA KICHWANI ZINAANZA KUYEYUKA.

CAPO.
 
Kuna ajenda gani kati ya Rais Samia na Vilabu vya Simba na Yanga?, Wanatumika kisiasa na kufanya kampeni kabla ya wakati

Kuna namna CCM wanawatumia hawa wasemaji wa vilabu hivi pendwa nchini kujinufaisha kisiasa kipindi hiki kuelekea Uchaguzi, badala ya kuwekeza nguvu kwenye miradi ya maendeleo na kugusa maisha ya watu wa chini wakidhani labda kutumia watu wenye nguvu ya ushawishi ndio kujizolea mashabiki wao, siku hizi mambo yamebadilika, watu wanauelewa kwani kinachotakiwa ni kubadili maisha moja kwa moja ya wananchi.

Sasa hivi vilabu hivi vimekubali kubeba ajenda za kisiasa hadi kufikia hatua wana print picha ya Rais Samia kwenye T-Shirt zao zikiwa na maneno eti “Watoto wa Mama”, haya mambo sidhani kama yana impact zaidi ya kuleta mpasuko tu wa mashabiki. Kiongozi kama ni mtendaji mzuri haina haja ya mbwembwe hizi ili kupata watu au kura.
Pia, Soma:
+
Simba na Yanga hutumika kuzima vuguvugu au kusahaulisha wananchi changamoto zao za kijamii
Huu ni usengerema kabisa kwa vilabu hivi vya Kariakoo.
 
Back
Top Bottom