Simba na Yanga mnatunza wapi kumbukumbu zenu?

jerrytz

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
5,975
Reaction score
4,266
Wadau,
Kwa kipindi cha miezi miwili sasa nimekuwa nikitafuta kumbukumbu za Klabu kongwe hapa nchi - Simba Sports Club na Dar Young Africans kwa ajili ya project ndogo katika uandaaji wa documentary itakayoitwa - Simba and Yanga : East African Soccer Giants.
Kwa kweli nilianzia kwenye makao makuu ya timu hizi lakini nilichokutana nacho ni vituko,
Tuanzie Yanga,
Baada ya kufuata taratibu zote nilikutana na muhusika ambaye aliniambia kuwa atanipatia mtu atakayenipa historia yote, niliondoka nikidhani kuwa labda huyo ndiye mtunza kumbukumbu.
Niliporudi siku ya pili nikakabidhiwa mtu ambaye alinitaka nikae ili anipe historia, nikaishiwa nguvu. Seriously, historia ya Klabu ipo kichwani kwa mtu?

Msimbazi, Simba

Hapo napo nilikutana na mtu naye akanipa habari kama niliyoipata Yanga, akanitafutia mzee ambaye alianza kueleza habari za Simba akidai kwamba ana kumbukumbu nzuri.
Nilichoka baada ya kumuuliza anipatie safu ya viongozi wa Simba kwa nafasi ya Mwenyekiti/Rais kuanzia mwaka 2000.
Hapo nilikutana na ubabaishaji wa kutosha.

Kwa matokeo haya, tumeamua kubadili documentary na kufanya kitu kingine.

Viongozi wa Simba na Yanga inabidi mjue tunaishi kwenye zama tofauti.
 
Tuna tatizo kubwa sana la kutunza kumbukumbu kwenye michezo hii hata kwenye vyama vyote vya michezo
 
Klabu wangeweza kutengeneza magazine,documentary kuhusu matukio ya kihistoria ya hivyo vilabu kwa kuwahoji viongozi, wachezaji na wanachama waliokuwepo wakati huo
 
Nimekusifu kwa ulichofanya paragraph ya pili kutoka chini.

Hizo timu za Kariakoo, acha tu. Kuna mchezaji wa timu moja ya kariakoo, zilitakiwa video zake ktk deal la kumuuza ughaibuni, hakuna. Tena ni mwaka jana na mchezaji yupo ktk kikosi msimu huu. Deal lilifia hapo.
 
Nenda maktaba ya taifa, tafuta kitengo cha kumbukumbu za magazeti (microfilm or microfiche),


Hii ni fursa ya kuanzisha biashara ya kuweka magazeti ya zamani kwenye Internet.
 
Hivi hizo klabu zina season reviews?
 
Huko nimekwenda na maktaba ya UDSM pia kote huko nilikusanya data za kutosha lakini hadhikidhi hitaji kamili.
Kuna vitu kama usajili wa wachezaji kwa misimu husika na gharama iliyotumika pamoja na mikataba hiyo siwezi kuipata kwenye magazeti.
Magazeti yanaripoti kimatukio zaidi ila documentary ni zaidi ya hayo.
Nenda maktaba ya taifa, tafuta kitengo cha kumbukumbu za magazeti (microfilm or microfiche),


Hii ni fursa ya kuanzisha biashara ya kuweka magazeti ya zamani kwenye Internet.
 
Usichoke mkuu ungeendelea kuunga-unga hivyo hivyo, angalau kupitia hiyo documentary yako tungepata pa kuanzia.

Hivi vilabu, vilikuwa na nafuu zamani maana viliongozwa na watu wasio na elimu kubwa kama siku hizi zinaongozwa na wenye madigrii na pesa, lakini ni ajabu zaidi miaka hii hata website bado ni mgogoro mkubwa.
 
Hiyo mitimu ni shida tupu,timu hazina website,hazina maktaba,hazina vyanzo vya mapato (zaidi ya makusanyo ya mlangoni) hazina hata viwanja vya mazoezi.
 
Utafiti wako unaweza kusaidia sana huko mbeleni,usikate tamaa kwa sasa unaweza kuwatafuta baadhi ya watu watakupa inputs ambazo naamini zitasaidia kutengeneza documentary yako.Hawa watu bado wapo hai watafute unaweza kupata kwa kuanzia

Yanga-Ally Mayay,Lunyamila,Stephen Nemes,Ken Mkapa,Shadrack Nsajigwa,Jakaya Kikwete,Tarimba Abbas,Abdul Sauko,Mama Karume,Leodgar Tenga,Mkwasa

Simba-Mwameja,George Masatu,Boniface Pawasa,Juma Kaseja,Azim Dewji,Kassim Dewji,Ismael Rage,Chris Magori,Julio,Renatus Njohole,Ulimboka Mwakingwe,Hassan Dalali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…