jerrytz
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 5,975
- 4,266
Wadau,
Kwa kipindi cha miezi miwili sasa nimekuwa nikitafuta kumbukumbu za Klabu kongwe hapa nchi - Simba Sports Club na Dar Young Africans kwa ajili ya project ndogo katika uandaaji wa documentary itakayoitwa - Simba and Yanga : East African Soccer Giants.
Kwa kweli nilianzia kwenye makao makuu ya timu hizi lakini nilichokutana nacho ni vituko,
Tuanzie Yanga,
Baada ya kufuata taratibu zote nilikutana na muhusika ambaye aliniambia kuwa atanipatia mtu atakayenipa historia yote, niliondoka nikidhani kuwa labda huyo ndiye mtunza kumbukumbu.
Niliporudi siku ya pili nikakabidhiwa mtu ambaye alinitaka nikae ili anipe historia, nikaishiwa nguvu. Seriously, historia ya Klabu ipo kichwani kwa mtu?
Msimbazi, Simba
Hapo napo nilikutana na mtu naye akanipa habari kama niliyoipata Yanga, akanitafutia mzee ambaye alianza kueleza habari za Simba akidai kwamba ana kumbukumbu nzuri.
Nilichoka baada ya kumuuliza anipatie safu ya viongozi wa Simba kwa nafasi ya Mwenyekiti/Rais kuanzia mwaka 2000.
Hapo nilikutana na ubabaishaji wa kutosha.
Kwa matokeo haya, tumeamua kubadili documentary na kufanya kitu kingine.
Viongozi wa Simba na Yanga inabidi mjue tunaishi kwenye zama tofauti.