Simba na yanga nani ana washabiki wengi?

Simba na yanga nani ana washabiki wengi?

Simba imeanza kupendwa miaka ya 2000+ yanga ilipendwa sana miaka ya tisini.

Ni vigumu kuwa na jawabu la moja kwa moja kuhusu stats za mashabiki wa hizi timu 2.

Sisi wa zamani kidogo tuwape experience yetu.
Miaka ya 70's - 80's Yanga walikuwa na washabiki wengi sana. Ni miaka ambayo mitaani au mashuleni mkitaka kutengeneza timu za kuigiza za Simba vs Yanga, Simba ilikuwa inapata deficit kwenye first 11 yake huku Yanga ilikuwa na uwezo wa kufikisha hata timu 2 zenye full first 11.

Elimu ya siasa wakati ule ambayo ilikuwa inaongelea sana uanzishwaji wa Yanga kama sehemu ya mapambano ya Waafrika kupata uhuru ilichangia. Halafu kulikuwa na Karume (r.i.p) factor pia. Wengine tukakuta wazazi wetu ni washabiki wa Yanga wa kutupwa - nadhani kutokana na historical circumstances.
So, wengi wetu tukajikuta tunashabikia Yanga kimkumbo.

Sijui trend ilivyoendelea baada ya miaka hiyo, lakini yawezakana Simba walianza ku-bridge hiyo gap kwenye miaka ya 90's na kuendelea.

Similarly, wengi wetu wa miaka ile ya ushabiki wa mpira kwa soka la England tukajikuta tunashabikia Liverpool kwani ndio ilikuwa kwenye peak then. Siku hizi najikuta katika wakati mgumu sana kuwaeleza wanangu kwa nini na-support timu ambayo wao wanaiita "dhaifu" ya Liverpool badala ya eti "miamba" Man U, Arsenal, etc.
 
Kimsingi kwa Tanzania Yanga ndiyo yenye mashabiki wengi zaidi ya Simba, Kwa Africa Mashariki sina data zozote.
 
Back
Top Bottom