*SIMBA NA YANGA NDIO ALAMA YA MPIRA WETU* 📝 Hemed Suya.

*SIMBA NA YANGA NDIO ALAMA YA MPIRA WETU* 📝 Hemed Suya.

Melick Rutta

New Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
1
Reaction score
0
*SIMBA NA YANGA NDIO ALAMA YA MPIRA WETU*
📝 Hemed Suya.
Wadau na familia ya mpira wa mpira nchini Habarini za Jion. Baada ya kukimbizana na pilika za kutafta mkate wa siku basi kama kawaida tukitulia tunapata burudani ya mpira.

◾Ikitokea ukasafir mpaka jiji la Paris, moja ya alama itakayoashiria umefika Paris basi ni kupiga picha kwenye Mnara wa Paris. Ndio unafikaje Paris bila kupiga picha kwenue sehemu ambayo ni alama ya Paris na Ufaransa kwa ujumla?

🔹 Au ukisafir basi kwenda kwa Madiba pale Bondeni yaan South Africa basi walau upige picha kwenye sanamu la Mzee Mandela kuashiria kwamba kweli umefika South Africa.
*Ndio kila mahala pana alama zake*
🖋 Kwenye soka letu nchini hapana Shaka Simba na Yanga ndio alama za soka letu. Huwez ukakaa na kulizungumza soka la Tanzania bila kuvigusa vilabu hv kwa mazuri au kwa mabaya. Kwa miaka zaid ya 80 ya vilabu hivi vimejikita na kutengeneza alama ya vyenyewe kuwa alama ya soka letu.
🖊Leo nchini hakuna shabiki wa mpira ambaye hashabikii aidha Yanga au Simba. *Hakuna*
✒ Huwez kukuta eti mtu anashabikia Azam au Singida United lkn moyon hana mapenzi na Aidha Simba au Yanga. Hata wachezaj wanaocheza team mbali mbali nchini nao ni mashabiki wa moja ya team hz.
🖋 Sasa kitendo hiki kwa baadhi ya watu na waandishi wa habar Tanzania wanakiona kama ni hasi kwenye soka letu. Wameishi wakiwaaminisha watu itikadi ya Simba na Yanga ni jambo baya. Kwa miaka kadhaa wanapambana na hili na bado halifanikiwi. Najiuliza kwa nn wasione uzur wa itikadi hii na kuitumia kama alama ya kunyenyua soka letu?
🖋 Trh 04/08/2019 uwanja wa taifa ule wenye kubeba watu elf 60 ulitapika rangi za njano na kijan na siku 2 baadae yaan trh 06/08/2019 uwanja huo huo ukatapika rangi nyekundu na nyeupe. Hiki kilikuwa ni kitendo cha kipekee kabisa ktk soka kusini mwa jangwa la sahara haijawah kutokea.
Je tuone hii itikad ya hv vilabu ni mbaya? Kwa nn tusione uzur kutokana na vilabu hv kwenye soka letu? Nchi zote za jirani zilizokuwa zinafuatilia matukio haya kwenye tv na kwenye mitandao walionyesha kushangazwa na kuvutiwa sana na matukio haya. Je ni kweli hatuon mazuri ya Haya?
🖋 Simba na Yanga ni alama za mpira wetu. Ifike kipindi tubadilike na kuona mazur ya alama hii katika soka letu. Tutumie jitihada ya kutumia alama hz kukuza na kunyenyua soka letu nchini. *Ifike kipindi Tuzitunze na kuzienzi alama hizi kwenye soka letu*

✍🏾Hemed Suya
Kibaoni Singida.
0717161366.
 
Hizo team zingekuwa zinaendana na maendeleo ya jins zinavyojulikana lakin ni hovyo tu sioni cha kujivunia kwa Simba na yanga zaid ni kudidimiza soka letu may be waanze kubadilika na maendeleo tuyaone la sivyo ni alama ya hovyo kwa taifa...team zinamiaka 80 na mashabik wengi lakin hazina chochote cha maendeleo au ww mkuu unayaona? Hata uwanja tu hapana ,angalia azam ya juz tu lkn inakila kitu ,academ,uwanja,biashara za team,
 
Yanga ndio alama ya Taifa, ndio timu iliyoanzishwa na waafrica wazalendo waliopigania uhuru. Simba ilianzishwa na wahindi na waarabu vibaraka wa wakoloni
 
Nasikia ndio wanaongoza kwa "mabenchi ya ufundi"
 
Yanga ndio alama ya Taifa, ndio timu iliyoanzishwa na waafrica wazalendo waliopigania uhuru. Simba ilianzishwa na wahindi na waarabu vibaraka wa wakoloni
Kuwa basi na ushabiki wenye manufaa mjomba, kuliko kuongea pumba.

wewe unaijua istoria ya simba sc? Tuulize sisi tutakujuza kijana wewe ni kijana wa mihemkotu hujui istoria ya timu hizi vizuri.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom