babacollins
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 901
- 212
Pamoja na kubezwa mara kwa mara, kupondwa na wakati mwingine baadhi ya watu kutoa wito wa vilabu hivi vikongwe vitoweshwe kwenye ulimwengu wa soka kwa kudaiwa kwamba vinadidimiza mchezo wa soka, ni ukweli usiopingika vilabu hivi viwili ni dhahabu mchangani kwa maendeleo ya soka na nchi kwa ujumla.
Mpaka sasa vimewavuta maelfu ya watu kujiingiza kwenye soka, vimeongeza umaarufu wa vyombo vingi vya habari na wanahabari wenyewe, vimeingiza mabilioni ya pesa kupitia viingilio vya getini na wadhamini, maelfu ya vijana wamepitia katika vilabu hivi kama wachezaji na baadhi yao kuboresha maisha yao na wakati mwingine vimetumika hata kuleta utulivu na amani. Huu ni baadhi tu ya utajiri kwenye vilabu hivi.
Kifupi Simba na Yanga ni vilabu kiongozi kwenye soka la Tanzania. Viongozi wanaojiingiza katika vilabu hivi wana nafasi kubwa ya kuendeleza vilabu hivi na kuacha " legacy" ya "watu" na "vitu" kwenye vilabu hivi na kuendelea kuvuna utajiri tele uliopo kwenye hivi vilabu, jambo ambalo litaendelea kuvuta wengi kwenye soka na hata wengi kuingiza fedha zao na kuwekeza kwenye umiliki wa vilabu na kuwa na sekta bora ya michezo kupitia soka.
Mchezaji kiongozi.