Simba na Yanga wawaombe radhi Wazanzibari

Simba na Yanga wawaombe radhi Wazanzibari

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mashindano na sherehe za mapinduzi cup yamedoda kutokana na Simba na Yanga kutolewa kwenye hatua za awali za mashindano. Wanasiasa, wanamichezo, wadhamini na wazanzibar wote hawakutendewa haki na Simba na Yanga kupeleka timu dhaifu kwenye mashindano.

Shamrashamra hazitauwepo kamà nusu fainali na fainali hakuna Simba na Yanga, Simba au Yanga.

Viongozi wa hivi vilabu vya Simba na Yanga wahojiwe na wapewe adhabu kwa kuyadharau mashindano.
 
Mashindano na sherehe za mapinduzi cup yamedoda kutokana na Simba na Yanga kutolewa kwenye hatua za awali za mashindano. Wanasiasa, wanamichezo, wadhamini na wazanzibar wote hawakutendewa haki na Simba na Yanga kupeleka timu dhaifu kwenye mashindano,

Shamrashamra hazitauwepo kamà nusu fainali na fainali hakuna Simba na Yanga, Simba au Yanga.

Viongozi wa hivi vilabu vya Simba na Yanga wahojiwe na wapewe adhabu kwa kuyadharau mashindano.
Upumbavu wa mashabiki kuzigeuza Simba na Yanga kuwa zaidi ya imani za dini, umepelekea timu hizo kufanya zinachokutaka
 
Hii mapinduzi ni kupoteza muda tu, ndiyo maana hata Timu zinapeleka vikosi kufanya mazoezi tu.......
 
Pesa yenyewe inayogombaniwa ni 20+ M. Yani matumizi ya timu ni makubwa kuliko hata hicho wanachogombania. Nani apoteze nguvu na resources zake kijinga hivyo?
Wangekataa kushiriki, kwani kushiriki ni lazima?
 
Simba yanga
Daimondi konde
Mambo ya udaku
Imewafanya watu kuwa ovyo

Ova
 
Mashindano na sherehe za mapinduzi cup yamedoda kutokana na Simba na Yanga kutolewa kwenye hatua za awali za mashindano. Wanasiasa, wanamichezo, wadhamini na wazanzibar wote hawakutendewa haki na Simba na Yanga kupeleka timu dhaifu kwenye mashindano,

Shamrashamra hazitauwepo kamà nusu fainali na fainali hakuna Simba na Yanga, Simba au Yanga.

Viongozi wa hivi vilabu vya Simba na Yanga wahojiwe na wapewe adhabu kwa kuyadharau mashindano.
Ujinga wa kujitolea bila pesa uhuni waalike na timu zingine
 
Kama walivyo mjibu Mwakinyo,
itoshe kusema,
"Kombe la mapinduzi ni kwa ajili ya kuwanufaisha wazanzibari."
Inavyoonekana Kuna nguvu kubwa ya lazima inayovisukumiza vilabu kushiriki kwenye mashindano ambayo haviyataki, yanayowatia hasara kifedha, kimuda na kuwazalishia uchovu na majeraha kwa wachezaji wao. bila sababu za msingi. Hii inasababisha Simba na Yanga kupeleka benchi la ufundi na wachezaji hafifu kwenye mashindano ambayo yanawaharibia ratiba na mioango Yao kwenye mashindano mengine yanayowakabili.

Zanzibar walijiondoa kwenye ligi ya Tanzania (super league)
 
Ujinga wa kujitolea bila pesa uhuni waalike na timu zingine
Yule Masingisa Mbatta aliondoka Yanga na malalamiko ya timu kuendeshwa kisiasa zaidi kuliko ki professional. Timu inakwendaje kwenye mashindano yanayowatia hasara? Yanayominya muda wa maandalizi ya mashindano mengine? Yanayozalisha majeruhi? Yanayokula muda wa kwenda preseason?

Kosa lao ni kukubali kushiriki halafu hawaendi kushiriki bali kuhudhuria.
 
Kombe la kisiasa linaendeshwa kihujuma hata ukituzama baadhi ya mechi mfano

Namungo na aigle noir yaani namungo alibebwa sana na ndio maana linakosa wageni hilo kombe

Tuzo za wachezaji nyingi anapewa Mzanzibari

Refa anabeba baadhi ya timu

Timu za Zanzibar wanacheza rafu sana mfano kmkm na singida big stars yaani mchezaji unamvuta mwenzako hadi unachana jezi na hakuna kadi wala nini

Sasa nani apeleke kikosi chake akaumiziwe wachezaji wake

Kombe lenyewe halina thamani

Yaani bora simba na Yanga walivyotoka hata Azam nae angetoka tu mapema na lingepoa hilo [emoji3]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom