Simba na Yanga; Zama za Upinzani Usio na Tija, Zimekwisha!

Simba na Yanga; Zama za Upinzani Usio na Tija, Zimekwisha!

Baba Kiki

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2012
Posts
1,544
Reaction score
943
Baada ya kutumia karibu majuma matatu hivi tukijadili vituko vya soka letu vinavyochangiwa kwa kiasi kikubwa na usimamizi dhaifu wa soka na ushabiki usio na tija wa wafuasi wa timu hizi kubwa na kongwe zaidi nchini, leo tujaribu kuja kivingine ili kuinua soka la nchi hii.

Simba na Yanga ni timu kubwa zaidi za soka ktk nchi hii zenye historia kubwa sana ndani na nje ya Tanzania, na kwa vyovyote vile umaarufu wa klabu hizi ulipaswa kuendana na hali ya maendeleo ndani na nje ya uwanja.

Lakini pamoja na kuwa na mamilioni ya wafuasi, historia kubwa na uzoefu wa ligi na mashindano ya kimataifa, ni ukweli kuwa klbu hizi hazijakidhi haja ya wafuasi wake hasa katika maendeleo mfano mzuri ukiwa ni ukosefu japo wa viwanja vya mazoezi.

Zimetolewa sababu nyingi kwa nini klabu hizi haziendelei huku lawama zikitupwa kwa viongozi kwa kuendekeza maslahi binafsi na wanachama wasiojitambua. Yawezekana kuna ukweli ktk hili lakini ukiangalia kwa jicho la tatu utagundua kuwa kuna sababu nyingi zaidi kuliko viongozi tu. Mojawapo ya sababu inayozifanya timu hizi zibaki kama zilivyo miaka nenda miaka rudi ni KUTOKUSHIRIKIANA KTK MAMBO YA MSINGI. Zimebaki kushirikiana kwenye misiba na harusi tu, japo sio vibaya lakini haitoshi.

Licha ya upinzani wa jadi uliopo baina ya timu hizi, viongozi wa timu wangeamua kuwaongoza wananchama wao kuanzisha miradi ya pamoja inayoweza kuwasaidia kujiendeleza kuliko kila klabu kusimama kwa miguu yake kitu ambacho kimeonekana kuwa kikwazo kikubwa. Kwa mfano uwanja mkubwa wa mpira wa timu hizi unaweza kujengwa na makampuni kwa urahisi zaidi kama zinaweza kufadhiliwa kwa pamoja kuliko kila timu kutafuta mfadhili wake. Naamini hata kwa kutumia viingilio vya mechi wanazoandaa wenyewe huku wakihamasisha washabiki wao kuwaunga mkono zinaweza kuleta hata Mil 700 kila mechi ambayo yote inapelekwa kwenye ujenzi wa uwanja unaoleweka. Uwanja unaweza kuwa unabadilishwa jina kila moja kati ya klabu hizi inapokuwa mwenyeji kama vile mambo ya AC Milan na Inter kama alivyowahi kupendekeza mmoja kati ya wadau wa soka.

Tunaona jinsi TBL ilivyoweza kuzifadhili timu zote bila kuathiri upinzani uliopo, na pia tunaona baada ya Yanga kupata mfadhili mwingine ikashindikana hata kwa Simba kuendelea na ufadhili wa TBL. Pia tumeona Azam TV walivyong'ang'aniza dili la kuzipatia klabu zote za ligi kuu mgawo unaofanana kitu ambacho sio sawa lakini ni ukweli wametumia kutokuwepo kwa mshikamano baina ya timu hizi. Katika dili hili timu zote zinalaumiana, huku Yanga wakisema Simba walisaliti makubaliano, wakati Simba wakidai Yanga hususani M/Kiti wake hakuonesha jitihada ya kuboresha dili badala yake akawa anaonesha jeuri ya fedha.

Kwa jinsi hali ya uchumi ilivyo, na klabu hizi kuanza kutembeza bakuli, nawashauri ziungane ili kupata best deals za ufadhili hasa kwa Azam TV, Vodacom na kutafuta wafadhili wengine na ziachane kabisa na mpango wa fedha za hisani ambazo hazina uhakika.

Imetosha kuwa na ushibiki na upinzani usioleta tija kwa maendeleo ya klabu hizi. Klabu hizi zinazidi kuwa dhaifu kiuchumi lakini zimebakiza sifa tu za kukomoana kila anapojitokeza mhisani huku ukweli ukiwa ni mtegemea cha nduguye hufa maskini. Ninaamini kuna mengi ya kuwaunganisha nje ya uwanja kuliko kuwatenganisha. Umoja ni Nguvu Utengano ni Udhaifu.
 
hizi timu huwa hazishirikiani kwenye mambo ya msingi zikifikiria zinakomoa timu nyingine kumbe zinakomoana mikataba yote ya vodacom na Azam tv ambayo TFF inapata inapata kutokana na hizi timu lakini badala ya hizi timu kufaidika wanafaidika wachache huwezi ukalipa sawa mgawo wa tv kwa kila timu lakini muda wote unaonyesha live mechi za timu za simba na yanga na bado zitaendelea kuwa omba omba hadi pale zitakapopata viongozi wanaojitambua
 
Back
Top Bottom