Alpaslan Bey
Senior Member
- Nov 4, 2023
- 121
- 163
Ndugu wana JF,
Kwanza nikiri kuwa mimi ni shabiki wa Simba Sports Club Miaka 33 sasa.
Juzi nilikuwa Igurusi mkoani Mbeya kuna sehemu nilikuwa napata chakula. Eneo nililokuwepo nilikutana na wanachama na mashabiki wengi sana wa Simba sports club wakiwa wamevalia jezi za Simba huku wakiwa na bashasha na shauku ya mechi ya leo.
Baada ya kumaliza kula nilipotoka nje ndipo nilipobaini wingi ule ni kwa sababu gari yao (coaster) waliyokuwa wanatumia ilikuwa imeharibika na pale walisimama ili kufanya matengenezo na kuendelea na safari ya kwenda kushuhudia mtanange dhidi ya Yanga.
Nililojifunza ni kwamba
1. Mpira wa miguu hususani mechi za Simba na Yanga huwafanya watu kutumia gharama kubwa ya kusafiri kwenda kuziunga mkono timu zao na pengine ni kutoka kila kona ya nchi
2. Watu wanahatarisha maisha yao kwa ajili ya safari na hata likiwapata la kuwapata hakuna fidia ambayo wanapata kwa mapenzi yao kwa klabu
3. Watu wanaacha familia zao, wapendwa wao na biashara zao kwa maslahi ya klabu zao
Kwa haya machache, ikitokea mechi inaahirishwa kwa sababu ambazo kimsingi ni za kikanuni kwa nini yafikiwe maamuzi ya kuahirisha mechi?? Hatuoni kama tutakuwa tumewaumiza watu wengi sana ambao kwa namna moja ama nyingine wanakuwa wamepoteza??
Nadhani ni wakati sasa wa hizi klabu kubwa mbili kuacha ubinafsi na kufikiria maslahi mapana ya mashabiki wao na taifa kwa ujumla