Simba na Yanga zinaendeshwaje?

Simba na Yanga zinaendeshwaje?

TRABSOH

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
351
Reaction score
559
Wakuu habari

Katika miaka kadhaa na michache ya kuishi kwangu hapa duniani nmekuwa msomaji wa majarida na maandiko mbalimbali yanayohusu maendeleo ya miji, taasisi na nchi tofauti tofauti.

Moja ya vitu ambavyo nimeviona vipo katika halakati za maendeleo ya maeneo mbalimbali ni uchaguzi wa vision na mission ndani ya plan flani ,maendeleo ya taasisi yoyote yaliyotokea kwa kuwa na njia iliyochongwa na kuonesha tunatakiwa kupita wapi ili kufika wapi katika kipindi cha muda flani.

Mfano mamelord sundown katika eneo la kutafuta mashabiki wana programs ambazo ziko planned nini kinapaswa kufanywa kugain popularity na zina time limit, utaona mechi zao ni buree wanahitaji uvae jezi yao tu, lakini pia mashuleni wana programmes za kuongea na wanafunzi na kuwapa zawadi za jezi.

Simba na yanga ni vilabu vya michezo na vina maeneo mengi ya kuyafanyia kazi ili viweze kuwa katika hadhi ya vilabu vikubwa na venye mafanikio. Kimsingi hivi si vilabu vikubwa ukisema una asses vilabu vikubwa Africa havina tofauti na maskini aliyepata msaada wa kazi ya muda mfupi inayoweza kumpa kula na kunywa vizuri na akaona amefanikiwa.

Vilabu havina facilities wao ni kucheza mpira tuu, na kutaka mafanikio ya ndani ya pitch bila kujua maendeleo ya ndani ya pitch ni matokeo ya maendeleo nje ya pitch.

Kwa namna gani vilabu hivi vinaendeshwa? Je kiongozi kama hersi au try again na mangungu wakiingja madarakani wanafata mpango upi wa maendeleo ambao umekaguliwa na wataalamu na kupigiwa kura na wanachama kuwa ni mpango bora utakaowafanya kufika stage flani ya maendeleo.

Maendeleo nayozungumzia hapa ni miundombinu bora ya uendeshwaji wa klabu ndani na nje ya pitch, viwanja vya mazoezi, hostels, gym, club restaurants lakini pia ofisi zenye hadhi ya klabu kubwa sio majengo ya kumbukumb za torati pale kariakoo. Uwanja kwa ajili ya matukio ya klabu kama mechi.

Je vilabu hivi vina endeshwa katika mlengo upi wanaamini katika njia ipi yani wana management plans au vinaendaje endaje, kiongozi akichaguliwa anafata nini au anajichagulia tu cha kufanya.
Mashabiki ndio akili hawana kabisa wanakwambia tu sisi Timu ishinde tu, Timu inashindaje bila club kuwa na uendeshaji wenye msingi imara, leo Timu inaenda robo kesho inatolewa na ud songo mwingine ni bingwa wa kihistoria wa nchi lakini aliishi miaka 25 bila makundi ya klabu bingwa inashangaza.

Timu hazina viwanja ata vya watu 5000 zimeanzishwa 1925 sjui ni jambo la ajabu, kama mambo yangekuwa yanaenda kwa mipango jambo kama hili ni nadra kutokea, klabu za mpira hazina hata programme za vijana zinalazimishwa na Tff kuwa na Timu za under 20.

Hivi vilabu vinaendeshwaje?
 
Inafahamika Upande mmoja wenye akili ni wawili tu huku upande mwingine ni mbumbumbu hapo utegemee kuwe na develop plan[emoji848]
 
Mfano mamelord sundown katika eneo la kutafuta mashabiki wana programs ambazo ziko planned nini
Usifananishe team ya Afrika kusini na team za Afrika mashariki kimkakati, wala Usifananishe Uchumi wa Afrika kusini na nchi za Africa mashariki, wametuzidi mbali sana.

Tafadhali fananisha team za nchi za Africa mashariki kwa Africa mashariki utaeleweka.
 
Hebu tingisha kichwa kidogo hivi. Unahisi nn?
 
Usifananishe team ya Afrika kusini na team za Afrika mashariki kimkakati, wala Usifananishe Uchumi wa Afrika kusini na nchi za Africa mashariki, wametuzidi mbali sana.

Tafadhali fananisha team za nchi za Africa mashariki kwa Africa mashariki utaeleweka.
Yani plan nazo zinataka nguvu ? Plan si inapangwa kutegemeana na rasilimali hatuwezi kuwa kama wao lakini tuwe na njia zetu kivyetu vyetu , tujifunze kwa gormahia? unajifunza kwa aliye endelea au unayefanana nae hali?
 
Ifikie wakati hivi vilabu viachwe kutumika kama madaraja ya watu wachache kujinufaisha kisiasa na pia kiuchumi.

Viongozi wa hivi vilabu wanatakiwa wajikite pia kwenye kutekeleza ahadi zao za kuimarisha miundombinu ikiwemo ya viwanja, hosteli za wachezaji, nk. na siyo kwenye vikombe tu.
 
Usitake tufanane

Mamelodi wanatafuta mashabiki, Tz ukizaliwa tu you are either Simba au Yanga, sasa tuhangaike kutafuta nn tena? Figo au utumbo?
Umeelewa nilichoongeaa kweli? 'Mfano hutumika kueeleza jambo gumu katika namna nyepesi' elewa hii sentensi
 
Ifikie wakati hivi vilabu viachwe kutumika kama madaraja ya watu wachache kujinufaisha kisiasa na pia kiuchumi.

Viongozi wa hivi vilabu wanatakiwa wajikite pia kwenye kutekeleza ahadi zao za kuimarisha miundombinu ikiwemo ya viwanja, hosteli za wachezaji, nk. na siyo kwenye vikombe tu.
Wakati huo utaletwa na nani sasa
 
Zinaendeshwa kama mnavyoendesha Tanesco, TTCL na idara zingine za umma. Hao ni jamii ile ile ya ngozi nyeusi kwenye mambo ya umma kujali tumbo lake tu. Ili zipate maendeleo ya nje ya uwanja labda ziuzwe kwa watu binafsi na kuachana na wanachama njaa wanaoridhika kupikiwa supu , kupikiwa pilau na kuletewa Manzoki kwenye uchaguzi.
 
Timu za wananchi sheria azitaki ziuzwe 100% si unaona mambo ya mo 49%
 
Mafanikio ya kwenye pitch SI Yana akisi mafanikio nje ya pitch? Huoni wananchi wanavyo ng'ara kwenye pitch?
 
Back
Top Bottom