Wakuu habari
Katika miaka kadhaa na michache ya kuishi kwangu hapa duniani nmekuwa msomaji wa majarida na maandiko mbalimbali yanayohusu maendeleo ya miji, taasisi na nchi tofauti tofauti.
Moja ya vitu ambavyo nimeviona vipo katika halakati za maendeleo ya maeneo mbalimbali ni uchaguzi wa vision na mission ndani ya plan flani ,maendeleo ya taasisi yoyote yaliyotokea kwa kuwa na njia iliyochongwa na kuonesha tunatakiwa kupita wapi ili kufika wapi katika kipindi cha muda flani.
Mfano mamelord sundown katika eneo la kutafuta mashabiki wana programs ambazo ziko planned nini kinapaswa kufanywa kugain popularity na zina time limit, utaona mechi zao ni buree wanahitaji uvae jezi yao tu, lakini pia mashuleni wana programmes za kuongea na wanafunzi na kuwapa zawadi za jezi.
Simba na yanga ni vilabu vya michezo na vina maeneo mengi ya kuyafanyia kazi ili viweze kuwa katika hadhi ya vilabu vikubwa na venye mafanikio. Kimsingi hivi si vilabu vikubwa ukisema una asses vilabu vikubwa Africa havina tofauti na maskini aliyepata msaada wa kazi ya muda mfupi inayoweza kumpa kula na kunywa vizuri na akaona amefanikiwa.
Vilabu havina facilities wao ni kucheza mpira tuu, na kutaka mafanikio ya ndani ya pitch bila kujua maendeleo ya ndani ya pitch ni matokeo ya maendeleo nje ya pitch.
Kwa namna gani vilabu hivi vinaendeshwa? Je kiongozi kama hersi au try again na mangungu wakiingja madarakani wanafata mpango upi wa maendeleo ambao umekaguliwa na wataalamu na kupigiwa kura na wanachama kuwa ni mpango bora utakaowafanya kufika stage flani ya maendeleo.
Maendeleo nayozungumzia hapa ni miundombinu bora ya uendeshwaji wa klabu ndani na nje ya pitch, viwanja vya mazoezi, hostels, gym, club restaurants lakini pia ofisi zenye hadhi ya klabu kubwa sio majengo ya kumbukumb za torati pale kariakoo. Uwanja kwa ajili ya matukio ya klabu kama mechi.
Je vilabu hivi vina endeshwa katika mlengo upi wanaamini katika njia ipi yani wana management plans au vinaendaje endaje, kiongozi akichaguliwa anafata nini au anajichagulia tu cha kufanya.
Mashabiki ndio akili hawana kabisa wanakwambia tu sisi Timu ishinde tu, Timu inashindaje bila club kuwa na uendeshaji wenye msingi imara, leo Timu inaenda robo kesho inatolewa na ud songo mwingine ni bingwa wa kihistoria wa nchi lakini aliishi miaka 25 bila makundi ya klabu bingwa inashangaza.
Timu hazina viwanja ata vya watu 5000 zimeanzishwa 1925 sjui ni jambo la ajabu, kama mambo yangekuwa yanaenda kwa mipango jambo kama hili ni nadra kutokea, klabu za mpira hazina hata programme za vijana zinalazimishwa na Tff kuwa na Timu za under 20.
Hivi vilabu vinaendeshwaje?