bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,679
Sina shaka kusema Simba ndio kati ya timu zenye kashfa za kuhonga wachezaji au marefa hapa Tanzania.
Ukianza saga la Kabwili hili liliisha bila kujua hatima yake, Kabwili aliyewahi kuwa golikipa wa Yanga kipindi kile cha kina Kindoki aliwahi kuripoti kuhusu kuhadiwa gari na viongozi wa Simba endapo lengo lao lingetimia la kumwadaa kijana awachie magoli kati ya mechi ya Simba na Yanga.
Sakata hili lilikua la moto sana mpaka kupelekea Tff kuingilia kati na kulizima, ila ingekua nchi za wenzetu sio ajabu uchunguzi wa nguvu ungefanyika na Bila Shaka lingekua ni ukweli tu kwa kuangalia historia za nyuma za Simba, kumbe basi leo hii Simba isingekuwepo au wangeshushwa daraja la 5 huko washukuru busara za Tff kuficha uchafu.
Nakumbuka pia kuna mchezaji wao wa zamani Ulimboka naye aliwahi kuwa na kashfa ya kutumika na Viongozi wa Simba kwa kumpa fedha ili azigawe kwa wachezaji wa timu pinzani ili wapate matokeo ya mserereko hili nao Tff/FAT walilifumbia macho.
Haya ni yale yanayojulika je yasiyojulikana ni mangapi, ni vema Simba wakaachana na matukio ya kuaibisha soka letu na kujikita kwenye kucheza mpira.