Simba ni team au kikundi cha wastaafu?

Simba ni team au kikundi cha wastaafu?

Wakuu naangalia marudio hapa ya mechi ya simba na prison.

Naona hapa simba wamechomoa goli dakika hizi za lala salama
Tukiendelea hivi chama atachomoa labda iwe mbili kwa mbili!

Ila sasa huu utaratibu wa kupanga wazee kwenye team unatuumiza sana wakuu ..

Hapa unakutana na mzee mwenzangu baba esta mbavu ya kulia...miaka 35.

Kushoto mzee mwenzangu mwenyewe mwenda yeye kidogo ana 28.

Kati pale unamkuta mzee mwenzetu mstaafu bwana ngoma miaka 61..

Mbele kabisa unamkuta mzee wetu chama miaka 60.

Pembeni unamkuta mpigania vita ya Uhuru Burundi bwana saidi ntombonkiza miaka 85..

Mbele kabisa anasimama mzee wetu bwana omary mwaijobe miaka 65

Sasa wakuu hamuoni tunaomuia ni sisi mashabiki eeh? Hawa si wastaafu kabisa wanakula pension? Why mnawapanga?

Mnaona yalitokea Leo kwa maafande kuwapigisha kwata wazee hawa mnataka msiba?

Wakifa nani atatushauri vijana jamani? Nilimuona kabisa kapombe anaomba maji pumzi imekata miguu imekakamaa .


Simba fanyeni usajiri..
Aaahaaa
 
Nimeangalia zaidi ya mara mbili kujua kilichosababisha Inonga alale chini. Nilijua aliguswa labda kulikuwa na faulo, kumbe aisee kalambwa chenga moja matata sana hadi chini.
Magwangala bado anakwambia kitasa hiko..!
 
Sasa kama picha hii ndio inatumika kumdiscredit Inonga wewe utakuwa na matatizo makubwa zaidi ya anayotueleza Manara juu ya washabiki wa utopolo!
Kwahiyo kazi yake uwanjani ilikuwa ipi wewe mstaafu mwenzie?
 
Kwahiyo kazi yake uwanjani ilikuwa ipi wewe mstaafu mwenzie?
Bila shaka wewe bado mtoto wa 2000,hujawahi kumwona Vidick akipigwa chenga na Torres na haikuondoa ubora wake,Van Dyke anapopigwa chenga na Samata inaondoa ubora wake?Huyo Inonga ndiye mchezaji pekee kuwahi kucheza nusu fainali ya AFCON kutoka kwenye ligi yetu,hiyo najua unajivunia hata kama wewe siye JK au Mzee Manara
 
Back
Top Bottom