Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Hii ni timu tishio kwenye kundi lao kwa sasa, inacheza direct football ikiwatumia wachezaji wao hatari wenye kasi na nguvu kusukuma mashambulizi mbele, ni timu yenye beki imara sana wakiongozwa na beki kijana bwana joash onyango, Na ilo limeonekana kwenye mechi zote mbili walizocheza na timu ngumu sana ya vipers kutoka Uganda.
Pongezi nyingi sana ziende kwa bilionea anayewezesha pesa za usajili bwana Mo kafanya kazi kubwa sana kusajili wachezaji wakubwa wakina Sawadogo, Baleke, Kapama na wengineo wanaoifanya simba iwe tishio Afrika, Kiufupi nawaona simba mbali sana kwenye hii micheZo ya klabu bingwa Afrika na nawaona Horoya wakiacha alama zote kwa mkapa kutokana na mpira mkubwa wanaocheza hawa vijana wa Robertinho.
Timu iko vizuri sana kuanzia beki, viungo na washambuliaji kwakweli wamekamilika kila idara, Mashabiki wake ndio maana awana wasi wasi kabisa na timu yao, wanakula kuku kwa mrija stress kwao ni mwiko, Nawashauri sana wasiivuruge timu hii waiache ivyo ivyo ili wasije wakaaribu mipango ya kocha kufika nusu fainali au fainali ya klabu bingwa ambayo ndiyo ndoto ya kila mwanasimba wakiongozwa na mwenyekiti wao Bwana mangungu, Mama alitakiwa awaongeze mil.5 nyingine kwa pira lile la jana dhidi ya vipers ambao walipelekewa moto wa gesi mwanzo mwisho kudadadeki, Mwisho kabisa pongexi ziende kwa viongozi wote waliofanikisha kuitengeneza simba tishio inayoweza kuifunga timu yoyote nje ndani kama walivyofanya kwa vipers!