Simba: Ondoa Barbara Matola weka Magori

Simba: Ondoa Barbara Matola weka Magori

bulabo

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
628
Reaction score
780
Bila kumungunya maneno. Pale Simba aondoke barbara arudishwe magori. Haiwezekani Simba mechi tatu na mtani sisi wa kufungwa tu. Matola pia ni kichomi pale kuendelea kuwapanga akina mkude mzamiru watu hawana pass za mbele tumeumia tena msimu huu. Barbara tangu amekuwa CEO hatujapata kikombe chochote.

Akina kaduguga wamewatenga wakati ndo wababe w derby. Why kapombe anawekwa nje why phiri hachezi unamuanzisha kyombo ambaye ni mchezaj wa kawaida sana.

Uchawi ni sisi wenyewe wanasimba wachezaj wazuri wapo ila hatuwaamini huu ni uchawi na mchawi ni matola na menejimenti ya Simba

Hawaumia Simbi kupoteza na Yanga mara tatu

Sehemu ya mazoezi ya Simba iko wazi mno kila mtu anaona

Bila Simba kumuondoa barbara tumeumia tena msimu huu hana mipango ya ushindi zaidi ya kupiga picha na akina eto.

Moo na wenzake wakipita kwenye huu ukurusa ondoeni barbara mkude mzamiru rudisha HD. Wapenu wachezaj nafasi wenye uwezo kocha huyu akiendelea hivi hafiki octoba nawaambia.

Simba bila kubadilika why game za Yanga simba wanaonekana wanyonge sana hii ni cancer. Simba ya hasan dalali ilikuwa on fire kuliko hata hii tuna pesa
 
Mdhungu kaja na bundi kolokoloni mtajuta Sana msimu huu.

Shida ya Simba sio Matoka Wala Babra shida ya Simba ni Muhindi bahili !!!!!!!! Mudi ndio kirusi simba Kuna siku mtakumbuka maneno Yangu.

Wameshasema wengi me nakazia tena wanachama Kigwangala,Rage na wengine

Tuendelee kuwepo musa ni mwalimu mazuri Sana .

Bado geita anakuja kupiga kwenye mshono...

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kumbe kufungwa kunauma hivi! Sasa Matola na huyo Barbra wana makosa gani! Mara Inonga amehongwa!! Kazi kweli kweli.
 
Mqnchester wanajipigia tu huko pamoja na kubadili makocha. Simba ifanye jambo la tofauti.
 
Tatizo la uongozi.
1. Kuuza wachezaji wazuri halafu kununu wa viwango vya chini zaidi.
2. Kuchelewesha mno maamuzi kama vile mikataba, suala la jezi, uwanja wa mazoezi hauna uzio hadi sasa, na kuangalia sana suala marketting na branding, kusahau matokeo uwanjani - mwishowe bila matokeo biashara itakufa, kuachana na wazee au friends of Simba ( hizi timu zina mila zake) kutenga pesa za nje ya uwanja , Tanzania bila hivyo huwezi.
3. Kocha wa CV kubwa ambaye hana uwezo kwa sasa kazeeka, hatufai killa mara kutafuta kocha wakubwa halafu wachezaji wa kawaida hutafika.
4. Uwekezaji mkubwa nje ya ya mpira wenyewe haitawezekana.

La kufanya.
Kwa sasa kusajili tena forward mmoja bass maana muda unaenda.
Kuzingatia haya ya hapo juu.
Kuweka pesa kwa watu wa fitna mipango kabla ya mechi kuwateua haraka sana na Babra awe zaidi marketing sio kabisa kwenye fitna za mpira hawezi anafuata vitabu na ethics, wakati mpira wetu una taratibu zake.
Kocha aendelee tu kwa sasa hakuna muda, mechi za muhimu ni sita za ligi kuu na mbili za klabu bingwa, picha yooote itajulikana.
Mpira wa Bongo,,,,,
 
Kila mtu anasema lake, hii yote ni matarajio makubwa kutokana na usajili, tunajua mmeumia sana ila jikazeni tu mtapoa.
 
Bila kumungunya maneno. Pale Simba aondoke barbara arudishwe magori. Haiwezekani Simba mechi tatu na mtani sisi wa kufungwa tu....
Huyuuuuu narudia tena huyoooo?

KKijuwaji na kina gubu hichii, kinajitangaza tu mitandaoni kutafuta mme.

Tusahau ubingwa kwa huyuuu
 
Forward Kyombo na Kibu ,ni kuwapa kazi waganga
 
Bila kumungunya maneno. Pale Simba aondoke barbara arudishwe magori. Haiwezekani Simba mechi tatu na mtani sisi wa kufungwa tu...
Matola kafanya nn makolo??mbona kila timu ikifungwa mnamlaumu legend wenu matola>???ikishinda mnakaa kimya!!kila wakati mnamfanya matola ndo mbuzi wa kafara!

Toeni hoja why matola hafai??YANGA tuko vzr na mtaendelea kuwa wateja wetu!!nadhani mmeona pass ile ya aziz Ki!!hahaha milioni 400 si mchezooo
 
Barbara' ndo kocha?

Yeye Kama kiongozi anasajili,analipa ada za usajili,analipa mishahara ,anawalipa makocha na staff wengine.
Barbara anahusikaje na matokeo ya uwanjani?

Matokeo ya uwanjani aulizwe kocha na wachezaji wake.
Babra pale hawez kusimamia Ile timu upo sahihi
 
Bila kumungunya maneno. Pale Simba aondoke barbara arudishwe magori. Haiwezekani Simba mechi tatu na mtani sisi wa kufungwa tu...
Simba kipindi cha miaka mitano ya mafanikio imeongeza kundi kubwa la mashabiki wajinga wajinga sana.
 
Back
Top Bottom