Simba SC 1-1 Tanzania Prisons | Mkapa Stadium | VPL

Simba SC 1-1 Tanzania Prisons | Mkapa Stadium | VPL

homeless1

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2020
Posts
427
Reaction score
950
Ligi kuu Tanzania Bara kuendelea Leo ambapo mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara wanaenda kukutana na Wajelajela walohamishia makazi yao Sumbawanga wakitokea Mbeya

Ikumbukwe ni match ya kulipa kisasi kwa simba ambao walipoteza match yao ya kwanza kwenye uwanja wa Nelson Mandela na ni muhimu kwa Simba kwani ushindi utawafanya kumsogelea Dar Young Africa ambae ana point hamsini na simba ana arobaini na tano

Wajela jela ni wataalam wa kutoa draw lakini naona kila dalili ya wao kupoteza dhidi ya mnyama anaetaka kulipa kisasi

Kaa hapa hapa kwa ajili ya updates za mchezo huu na ikumbukwe match ni saa 1 kamili usiku.

=======

00' Mwamuzi kashapuliza kipenga kuashiria mwanzo wa kusukuma gozi

18' Luis anajaribu nje ya 18 lakini inakuwa off target

26' Simba wanapata penati baada Medatus kuunawa ndani ya 18

28' Mugalu anapiga mkwaju wa penati na Jeremiah anaupangua, Simba 0-0 Prisons

42' Kadi nyekundu kwa Jumanne Elfadhil baada ya kuokoa mpira na mguu wake kushukia shingoni kwa Mzamiru Yassin.

45' Mlinda mlango wa Tanzania Prisons, Kisubi yuko chini

45+3' Kisubi anainuka lakini Free kick ya Luis inagonga ukuta

45+6' Mpira Mapumziko

45' Mpira umerejea

51' Kisubi yuko chini na anapewa kadi ya njano baada ya kuinuka na kadi ya njano kwa daktari

54' Prisons wanapata free kick

55' Goaaaaal, Prisons wanapata bao la kwanza baada ya Kimenya kupiga mkwaju wa Free kick ya chini chini.

65' Mugalu anaweka lakini nakuwa kwenye offside

66' Benard Morrison anaingia kuchukua nafasi ya Bwalya

68' Luis anajaribu lakini unapaa juu kidogo ya lango la Prisons

69' John Bocco anapiga kichwa mpira uliotoka kona lakini unakuwa 'off target'

90' Mpira umeongezwa dakika 5

90+1' Almanusura Mugalu asawazishe lakini mpira unapaa kidogo juu ya lango

90+5' Luis anasawazisha, Simba 1-1 Prisons

90+6' Mpira umekwisha
 
Nawashangaa mnaoina Prison timu, yani kubahatisha kuifunga Simba kule Sumbawanga mara moja ndio mnaiona "inajua" kama utopolo, hao leo hawatoki kwa Mkapa.
 
Kile kikosi cha SEAL kinachopangwaga kwenye klabu bingwa ndio leo sasa kitaupiga na wajelajela.
Yani Simba ushindi ni lazima do or die.
 
Kwa kweli leo Simba tuweke full mkoko. Mechi muhimu sana hii kwetu. Tuliyemwachia usukani wa ligi ameshachoka kutushikia, anataka kutukabidhi nafasi yetu sisi kama wenye mali.
 
Haji manara post yake kabla ya game hio saa 1


Screenshot_2021-03-10-14-16-47.jpeg
 
Leo hii nitacheka jamani[emoji38][emoji38][emoji38] jitu likifa nitacheka mimi[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Haaaaa wapi.
Dua la kuku alimpati mwewe.
 
Huyu asukile ana kiburi na kujisikia eti hamjui Miquisone!
Asee hii nchi ukiwa utopolo akili huwa zinahamia kwenye kamasi tu.
 
Back
Top Bottom