Christopher Wallace
JF-Expert Member
- Dec 8, 2015
- 1,479
- 3,788
CAF: SIMBA YAIFUNGA GENDARMERIE 4-0, YAINGIA ROBO FAINALI
Timu ya #Simba imefanikiwa kuingia Hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya US Gendarmerie kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, usiku wa Aprili 3, 2022.
Matokeo hayo ya michuano hiyo ambao ipo chini ya Shirikisho la Soka Afrika (#CAF) yameiwezesha Simba kufikisha pointi 10 katika Kundi D, mabao yakiwekwa wavuni na Sadio Kanoute, Chris Mugalu aliyefunga mabao mawili na moja Gendarmerie wakijifunga.
Timu nyingine iliyosonga mbele katika kundi hilo ni RS Berkane ya Morocco ambayo nayo imefikisha pointi 10 baada ya kuifunga ASEC Mimosas bao 1-0 ya Ivory Coast.
=============================
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya CAF Confedaration Cup, Simba Sc itashuka dimbani dhidi ya Us Gendarmerie katika dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 4:00 usiku.
Hiyo itakuwa mechi ya mwisho ya kundi D na Simba wanahitaji ushindi wa aina yoyote ili waweze kufuzu hatua ya robo fainali.
Endapo Simba itashinda watafuzu kwa hatua ya robo fainali huku pia wakisikilizia matokeo ya Rs Berkane Vs Asec Mimosas mechi ambayo nayo itapigwa saa 4:00 usiku Kwa saa za Afrika ya Mashariki.
Hii itakuwa mara ya kwanza Simba kucheza mechi saa 4:00 usiku jambo ambalo linatia mashaka kama mashabiki watajitokeza kwa wingi kulinganisha na hali ya usalama.
Je Simba wataweza kufuzu robo fainali? Majibu ni saa 4:00 usiku kupitia ZBC2