ToniXrated
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 1,134
- 2,993
Inashangaza sana mara baada ya beki aliyeisha makali yake, Joash Onyango kupeleka ombi la uhamisho kwa uongozi wa Klabu ya Simba, mambo yakaanza kubadilika kwa beki gwiji raia wa Ivory Coast Mohammed Ouatara, akaanza kusugulishwa benchi mfululizo.
Yaani toka kocha "Mzawa" Juma Mgunda atue Msimbazi, nafasi pekee anayoipata beki huyu imekuwa ni kukaa benchi tu. Huwa najiuliza, huyu beki Onyango anaogopwa pale Simba SC ama vipi?
Binafsi nikimlinganisha Ouatara dhidi ya Onyango naona kabisa Ouatara ni beki anayemzidi Onyango kwa mambo mengi mno. Kifupi jamaa ni beki haswa na combination yake na Inonga ilikuwa nzuri sana. Cha ajabu ni kuwa huyu Kocha Mgunda amekuwa akimpa nafasi ya nne katika chaguo lake la mabeki.
Hivi Onyango na Kennedy Juma wana nini cha kumzidi Momo Ouatara? Tuwe wa kweli, leo hii akija kocha yeyote kutoka nje anayejua mpira lazima atampa nafasi Ouatara dhidi ya hawa mabeki ambao wana spidi ya kobe na hawana hata udhibiti wa mpira achilia mbali kupiga tu pasi kuwa ni mtihani kwao.
Mgunda unajichongea kaburi lako mwenyewe kwa kuendekeza "Uzawa".