View attachment 2696770
Achana na Bonanza la jana. Leo saa 7 mchana kinashuka chuma kingine.
Tetesi zinasema viongozi wameamua kuvunja benki. Taarifa ni kwamba katika kambi Uturuki ametua kipa kutoka Brazil 🇧🇷 Jafferson Luis aliyetambulishwa kwa wachezaji wenzake, lakini jana saa 7 mchana, Luis Mkandaji Miquissone naye alitambulishwa.
Tofauti na ilivyoripotiwa jana kwamba Simba imemsainisha kipa Mcameroon Simon Omossola anayetokea Saint Eloi Lupopo ya DR Congo. Ukweli ni kwamba Wekundu hao wamebadili gia na kumvuta Mbrazili Jafferson Luis mwenye miaka 29 aliyetambulishwa jana kambini Uturuki.
Kipa huyo Bora amesajiliwa kutoka Resende na baada ya Simba kumpiga chini Mcameroon, ambaye awali alipewa nafasi kubwa. Kipa huyo anatua Msimbazi kushindania namba na Aishi Manula aliye majeruhi.