Simba SC hatutashiriki Kagame CUP, tunapumzika kwanza

Simba SC hatutashiriki Kagame CUP, tunapumzika kwanza

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Simba imetangaza kujitoa kwenye mshindano ya Kagame yanatotarajiwa kufanyika mapema Agosti jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa timu Simba, Abbas Ally amesema hawashiriki Kagame ili kutoa nafasi kwa wachezaji kupumzika.

“Tumetoka kwenye Ligi ya Mabingwa halafu tukaunganisha kucheza Ligi Kuu na sasa tumemalizia Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa kishindo kwa kutwaa ubingwa dhidi ya watani wetu.

“Wachezaji wanahitaji mapumziko hata kama ni kwa muda mfupi lakini itawasaidia kuweka miili sawa. Baada ya siku 10 za mapumziko watarejea kambini,” amesema Abbas.

Abbas amesema wamekuwa na misimu minne mizuri ikiwemo kuchukua ubingwa wa ligi mara nne mfululizo pia kutwaa ubingwa wa ASFC mara mbili mfululizo.

“Tumeweka historia ya kutwaa mataji na kumfunga mtani na kuchukua ubingwa mbele yake. Kwenye ligi walituvimbia ila kwenye ASFC tumechukua ubingwa kilaini ,” amesema Abbas
 
Wacha wapumzimke kazi yao imeonekana. Vikombe vipo, wale wasiokua navyo mwaka huu chance yenu iyo sasa, ila cha ajabu utopolo naye ataiga tu na kujiweka kando
 
Nimefuraishwa na maamuzi ya Simba kutoshiriki Kagame, michuano hiyo imepoteza uzito kwa sababu haina ratiba ya kueleweka pia hata mapinduzi cup wasingekuwa wanashiriki hayo ni mabonanza tu hayana umuhimu wowote
 
Wangetumia Simba B yenye mchanganyiko na wachezaji wasiotumika sana (Mkude, Ally Slim, Ndemla, Gadiel, Duchu, Kenned pamoja wapya kina Kibu, Walter Bwalya......)
Hapana lazima kutakua Kuna pressure kubwa hii team kubwa. Fikiria mapinduzi kilienda kikosi b pamoja na watu wa majaribio ila kelele mpaka leo. Wacha tupumue tu kidogo
 
Katika maamuzi ambayo simba wamefanya ya maana ni kuwapa mapumziko wachezaji. Hatuwezi tukawa tunashiriki tu mashindano ya hovyo
 
Wangetumia Simba B yenye mchanganyiko na wachezaji wasiotumika sana (Mkude, Ally Slim, Ndemla, Gadiel, Duchu, Kenned pamoja wapya kina Kibu, Walter Bwalya......)
Wanahitaji kupumzika pia
 
Back
Top Bottom