Simba SC ilibugi maeneo haya kiufundi katika kukabiliana na Yanga SC

Simba ni kama vile haina uongozi au viongozi hawana uchungu na timu. Hayo yote yaliyoelezwa hapo juu yamesemwa sana hapa jamvini lakini hakuna hatua zilizochukuliwa. Na jambo ambalo ni kubwa na baya kama halitafanyiwa kazi haraka ni hilo la staminia na kasi kwani Simba pamoja na kushinda baadhi ya mechi lakini timu ilikuwa inakata moto dakika kuanzia ya 60/65. Na hili nafikiri Gamondi na benchi lake walilifanyia kazi sana kwani dhahama ndio ilianzia mida hiyo hiyo.

Yanga alipoondoka kocha wa mzuri wa viungo wametulia wametafuta kocha wa maana wa viungo ukija Simba tangu ameondoka Zrane hakuna kocha aliyekuja kumzidi Zrane au walau tu anayemfikia kiwango chake. Badala yake viongozi kwa ushauri wa Robertino wameenda kuleta kocha wa viungo mwenye kitambi maana yake hata yeye mwenyewe hajimudu afya yake. Timu hata ikiwa na wachezaji wenye vipaji vya namna gani kama ilivyo sasa hivi Simba lakini kama hawana stamina basi timu itaonekana ya kawaida tu matokeo yake yatakuwa mabovu.
 
hakuna hata siku siku moja mzamiru aliweza kumdhibiti aucho,chama na saidoo umri umeenda na stamina hawana hawawezi katu kushindana na vijana wenye kasi wa yanga,kule tanga mliona.Nahisi sio kocha aliyempanga manula
 
Sio mechi ya derby tu kwa sisi wenye jicho la kimpira tulishaona matatizo kitambo sana. Kuna madogo mtaani huwa nawaambia wananikatalia sana. Simba ina matatizo makubwa sana kwenye backline na kiungo mkabaji. Mechi nyingi wanakua exposed sana ndio maana Gamondi alianza na viungo washambuliaji wengi
 
FACT
 
KWELI KABISA WASIPOANGALIA MAKUNDI HAWATOBOI
 
hakika game ilikuwa ni ngumu mno kwa upande wa mnyama ni suala tu la kusema asante Mungu coz kuna nafasi zilikuwa zinakoswa nyingi mnooo lasivyo tungesema mengine leo


Political is just liKe a war always, BOOST YOUR CONFIDENCE
[emoji16] NILIHESABU NAFASI ZILIZOKOSWA NI KAMA TATU HIVI.
 
hakuna hata siku siku moja mzamiru aliweza kumdhibiti aucho,chama na saidoo umri umeenda na stamina hawana hawawezi katu kushindana na vijana wenye kasi wa yanga,kule tanga mliona.Nahisi sio kocha aliyempanga manula
RAFU ZAKE MZAMIRU HUWA ZINAMTOA KWENYE RELI AUCHO.
 
Kweli kabisa alisema.
 
UMEMPIGA NA KITU KIZITO SANA HAWEZI KURUDI TENA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…