Simba ni kama vile haina uongozi au viongozi hawana uchungu na timu. Hayo yote yaliyoelezwa hapo juu yamesemwa sana hapa jamvini lakini hakuna hatua zilizochukuliwa. Na jambo ambalo ni kubwa na baya kama halitafanyiwa kazi haraka ni hilo la staminia na kasi kwani Simba pamoja na kushinda baadhi ya mechi lakini timu ilikuwa inakata moto dakika kuanzia ya 60/65. Na hili nafikiri Gamondi na benchi lake walilifanyia kazi sana kwani dhahama ndio ilianzia mida hiyo hiyo.
Yanga alipoondoka kocha wa mzuri wa viungo wametulia wametafuta kocha wa maana wa viungo ukija Simba tangu ameondoka Zrane hakuna kocha aliyekuja kumzidi Zrane au walau tu anayemfikia kiwango chake. Badala yake viongozi kwa ushauri wa Robertino wameenda kuleta kocha wa viungo mwenye kitambi maana yake hata yeye mwenyewe hajimudu afya yake. Timu hata ikiwa na wachezaji wenye vipaji vya namna gani kama ilivyo sasa hivi Simba lakini kama hawana stamina basi timu itaonekana ya kawaida tu matokeo yake yatakuwa mabovu.