Simba SC inahitaji REFORMS


Ni vitu vya hovyo, kuna kina kaburu, kaduguda wote hawa ni old school mentality hakuna
Jipya. Mpira wa sasa unahitaji
Vijana wenye new ideas

Kuna kina janabi …… hawa watu wa nini wazee hawana ishu au anaenda kuchoma watu sindano

Wabaki kuwa washauri

Somewhere hata MO ni sehem ya tatizo
 
Hao Simba unaowataja wafanye mabadiliko ni akina nani? Kwa mandate ipi?

Huenda wewe unaona tatizo kumbe hata unaohisi ndo tatizo na wao wanatafuta chanzo cha tatizo ni kipi.
 
Wakitemwa wote hao kwa mkupuo, timu itacheza playoff, ama muipe kazi TFF ya kubadilisha kanuni, waseme mwakani tunaongeza timu 2 ili ziwe 18 hivyo mwaka kuu hakuna timu itakayoshuka daraja kama ilivyowahi kutokea miaka ile ya katikati ya 80.
 
Sasa niambie kina Matola wana Mbinu gani za Kisasa za Kuweza kusoma Mchezo wa Kimataifa na kumtia Mchezaji na Kumuingiza mwingine ?Uwezo wa Makocha wa Kizawa ni mdogo!
Pia Usajili wa Vijana 3 chipukizi unatakiwa na Kocha Mgeni asiingiliwe…
Kina Raage na wenzake wanapenda wazawa ili wawatumie kwa masslahi yao!
 
Kweli kabisa. Timu imejaa kamati na mabaraza ya wazee kama chama cha siasa. Hao wazee wangetengewa platform yao ndani ya utaratibu wa upande wa wanachama na siyo upande wa Bodi au Management na ingewezekana kila baada ya miezi 3, Mwenyekiti wa Wanachama anawapelekea ripoti ya maendeleo ya klabu. Bodi ingebaki na wataalamu na wabobezi wa mpira, sheria, fedha, utawala, nk. Management ingeajiri na kuwa na watendaji zaidi na CEO awe na maamuzi ya mwisho katika utendaji wa kila siku wa timu.

Mo kakutana na kizingiti kwa sababu kuna tofauti za kimaslahi, elimu na kuaminiana kwa hiyo na yeye kageuka mswahili hadi sasa hauwezi kumtofautisha na hao wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…