Simba SC is somethingwrong somewhere

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,205
Reaction score
2,697
Haya tena wana Simba tumepigwa na kibonde Ruvu shooting,safari hii nyumbani kwenye kiwanja kizuri kabisa.

Nasema there is something wrong somewhere siyo bure, timu inayohudumiwa vizuri haiwezi kubali matokeo kama haya mfurulizo, sasa wanaSimba tuzame kwenye mahesabu ili tuibue hizi wrong somewhwre befare Kariakoo debby vinginevyo siku hiyo itabidi tukimbie kulala kwenye mibuyu ili kuficha sura zetu.

SOMETHING WRONG YA KWANZA NI MORRISON:
Kasajiliwa kwa mbwembwe sana tena kwa hera nyingi kawakuta waliokuwa wanafia timu eti wao wameonekana si mali mali ni Morrison, hahika Morrison ni kirusi ameharibu kabisa morale ya timu wafia timu wamepunguza kujituma, acheze yeye Morrison, nakumbuka hii iliwahi kuwakuta hata watani zetu Yanga walipomsajili kwa hela nyingi ELISHA JOHN wachezaji aliowakuta wakawa wanampa pasi zote ELISHA JOHN si yeye ndo kaonekana mchezaji? afunge yeye sasa, Nakumbuka Yanga walikubali yaishe.

SOMETHINGWRONG YA PILI NI HAJI MANARA
Maneno yamekuwa mengi mno, eti mpira biliani what is that, Mpira ni magoli siyo biriani. Baba yake Sunday Ramadhani Manala ndio mchezaji wa kipaji cha juu kabisa kutokea nchi hii ni kwa sababu alikuwa anafunga magoli, tena alikuwa anafunga magoli yanayohitajika kwa wakati mwafaka mfano goli la kuongoza TAIFA CUP Pwani na Morogoro alipangua ngome yote ya Morogoro mpaka kipa. Bao la kusawazisha Club bingwa Afrika Enugu Rangers vs Yanga DSM mwaka 1975. Alipangua ngome yote yenye beki ngumu ya Enugu akampa pasi iliyopimwa kaka yake Kitwana Manala bao la kusawazisha . kazi nzima alifanya Sunday. Bao la kusawazisha Yanga na ACCRA HEATS OF OAK. Wakiwa Yanga wako nyuma bao moja Sunday aliipangua ngome yote ya Accra heats na kusawazisha bao vingenevvvvvyo ilikuwa aibu kwao kwani mechi yenyewe ilikuwa ya kirafiki ambayo Yanga waliiomba sana. Sasa haya Maneno ya mpira biriani Haji anayapata wapi? Si akamwulize baba yake kama mpira ni biriani? . Kwa hiyo msemo huu ufe mala moja tena kuanzia leo.

Nakataa Simba wanajifungusha ili kuwahadaa Yanga ili waone Simba ni mteremko ili wapate ushidndi kwenye Kariakoo dabby . nani alikuambia timu inaweza kujifungisha kwenye ligi ambapo kuna point 3 mhimu? falisafa hiyo ni upuuzi mtupu.
 
Tungeshinda haya yasingekuwepo, Mpira ndo uko hivi Sasa, kukosa striker mzoefu kumeiadhibu Simba mechi mbili mfululizo.

Huyo Morrison kaleta ngao ya jamii, manara amekuwepo mda mrefu na tulifanikiwa bila tatizo, wachezaji Bado hatuna[emoji23][emoji23]

Sema tumepigwa tu, na tukimfukuza kocha Ni kosa kubwa Sana, inaumiza lakini ndo hivyo!.
 
Tuache mambo ya kinazi. Tumepigwa ndio. Mapengo ya wachezaji muhimu ndio yanaonekana.
Morrison kacheza mpira na umeonekana. Ajibu ni 🚮, katika sajili ambazo nilizipinga na naendelea kuzipinga ni ya huyu jamaa
 
Kwamba kusajiliwa kwa Morrison ndio kumeshusha kiwango cha Simba? Kwamba maneno ya Manara ndio yanafanya timu isishinde uwanjani? Mbona naona kama hakuna uhusiano! Nahisi umeandika tu bila utulivu. Angalia sababu za kiufundi, hizo ulizoleta sio kabisa. Kwanza hela ya usajili wa Morrison ni ndogo kabisa, ungejua
 
Tatzo ni kikosi kipana na kocha kuleta majaribu. Hii dhana ya kuwa tunakikosi kipana ndio kinatugharimu. Leo maingizo mapya karibia matano tofauti na mechi ya kule sumbawanga sasa unategemea hapo kombination inapatikana wapi.

Mwanzo wa msimu tulitegemea iwe vzuri zaidi kuliko yanga kwa maaana ni wachezaji wamekaa pamoja kwa muda mrefu ukilinganisha na Yanga lakini kinachotokea utadhani na Simba ni km yanga alisajili wachezaji nusu ya timu.

Kocha anashindwaje kuwa na kikosi cha kwanza cha kuaminika lkn mwishowi utadhani na yeye anatafuta kombination as if ni mgeni na kaingia msimu huu msimbazi. Tahadhari km kimataifa tunaenda hv naamini yanatokea ya msimu uliopita
 
Nikuweka mambo sawa tu kwenye benchi la ufundi.huyu kocha kama vipi apewe ruksa.
 
Beki line wajaribu kumpumzisha joash Achieng Onyango, wacheze Wawa na Kennedy Juma, pia Ame akicheza acheze na Wawa,

Onyango siyo mtulivu,

nb: pengo la Chama Ni ngumu kuliziba asipokuwepo uwanjani, striker mzoefu Ni mhimu Sana japo wako majeruhi [emoji26][emoji26][emoji26]
 
Tatzo ni kikosi kipana na kocha kuleta majaribu. Hii dhana ya kuwa tunakikosi kipana ndio kinatugharimu. Leo maingizo mapya karibia matano tofauti na mechi ya kule sumbawanga sasa unategemea hapo kombination inapatikana wapi...
Kocha kaweka hao kwa kukosa wazoefu wako majeruhi [emoji26][emoji26]
 
OKW BOBAN SUNZU nilikueleza kipigo anachokipata simba ni sawa na atakachokipata Tundu Lissu. Una mikosi mwaka huu ujue
 
Tatizo la kwanza Simba ni kochakwani hana plan b pia anakariri wachezaji wa kupanga na kuwaweka wengine benchi muda mrefu halafu hajui kufanya mabadiriko unamuachaje Ajibu hadi mwisho wakati hana impact yoyote na pia anachelewa kufanya mabadiriko.
Tatizo jingine ni wachezaji wa Simba kqma Mkude kiwango kimeshuka, Mzamiru hakabi, mipira mirefu isiyofikia walengwa, Shabalala kuchelewa kurudi kukaba, kutoa pasi boko, kulazimisha chenga wakati hajui.
Tatizo jingine ni uongozi waliacha wachezaji wazuri kama Deo Kanda, Shibob na kusajili ama kwa kuikomoa yanga na kusajili bila kuangalia mahitaji ya timu mwisho wachezaji wa Simba hawajitumi wanajiona kama mastaa wa bacelona ukiondoa Luis, Wawa, Onyango , Kapombe wengi walikuwa hawajitumi kugombania mpira
 
Kiukweli Jonas Mkude kiwango kimeporomoka mguuni ana kigugumizi halafu anapoteza mipira Sana.

Ajibu hatakiwi kubaki Simba Hana msaada, huo ndo ukweli.

Pia ndemla Bora angeanza na mzamiru akaingia baadae,


Kocha anachelewa Sana kufanya substitution.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…