Simba SC iuzwe kwa tajiri Dewji

Simba SC iuzwe kwa tajiri Dewji

Simba chama langu ila nahisi hata msimu ujao yebo yebo watatupiga mbili
 
Nyie ndio mashabiki Maandazi ambao hata kadi hamna mnakuja mitandaoni kupiga kelele eti simba iuzwe. Kwanza unamjua mmiliki wa Simba SC ni nani? . Simba ni mali ya wanachama hivyo kuuzwa ni swala ambalo haliwezekani. Pia mtumie akili si kila tajiri anayetaka Timu basi yupo tayari kuleta maendeleo wengine wanawahitaji kwa ajili ya Fanbase yenu ili wawatumie katika biashara zao kama marketing tool.

Kuleta Maendeleo si lazima ainunue timu kuna njia nyingi sana angeweza kuzitumia. angeweka mapenzi mbele zaidi ya kutafuta profit ya biashara zake kwa kutaka kuwatumia nyie mavyura FC kama mabango ya Matangazo.

Angejifunza kutoka kwa Manji. Ni Mpenda Michezo na Timu ya Yanga iko Moyoni mwake. Pamoja na kuwa na Hela nyingi kumshinda huyo MO hakutaka kuinunua yanga wala kuitumia katika biashara zake. Alijua kuwa Yanga kwa kipindi kile ilikuwa na migogoro kutokana na uongozi mbaya hivyo akaamua kuinusuru kwa kugombea uenyekiti kama mwanachama wa kawaida. Maendeleo tuliyonayo leo ni Mapenzi ya dhati aliyonayo Manji na viongozi wenzake kwa timu yetu. Kwa kipindi cha uongozi wake aliua kabisa nguvu za wazee wa yanga kina akili mali na kuwaunganisha wanachama na makundi yote yaliyokuwa yanatofautiana. Bila umoja hamtafika kokote na hicho ndicho alichotakiwa kukifikiria kwanza MO kama kweli anaitaka Timu.

Simba ya sasahivi imegawika kama ilivyokuwa Yanga enzi zile. Mna makundi ambayo hayana kichwa wala miguu. kila mtu anasajili wachezaji wake na wachezaji wanacheza kutokana na Matakwa ya Mabwana zao. Mlichotakiwa kukifanya sasahivi ili kuinusuru timu yenu ni kujitahidi kujenga umoja kwanza miongoni mwa wanachama wote wa Matopeni, Timu iendeshwe kisasa kama vile kuwa na kamati ya usajili ambayo itakuwa inaeleweka na sio kuacha kila mtu ajipe hilo jukumu mwisho mnahujumiana wenyewe kwa wenyewe, wanachama waelewe haki zao kuwa wao ndio wenye timu na sio kina aveva, huyo rais yupo pale kwa niaba yenu na mda wowote mna nguvu ya kumuondoa. Vunjeni makundi yote na muwe kitu kimoja ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi magumu ya kuwatimua kina Kaburu, hanspope na Magori kwenye timu yenu.

Nguvu mnazo na uwezo mnao, hakikisheni kila kilichotajwa kwenye katiba yenu kina tekelezwa na hilo jukumu msimuachie Bi. Hindu peke yake liwe jukumu la Mambumbumbu wote.

Mimi kama mwanachama wa Yanga nawatakia mafanikio mema katika haya majaribu mnayopitia. Ila Mwambieni MO kama kweli ana uchungu na Simba ailetee Mafanikio akiwa kama Mwanachama wa Kawaida na sio Kama Mmiliki. Kama Mbinu hana aseme tumuunganishe na Jemedari Yusuph Manji ampe Mbinu za Kivita.

Mkuu nyie mna mafanikio sana

Tuache Na Simba yetu

Endelea na Yanga Yenu yenye mafanikio kedekede

Tunayajua matatizo yetu kuliko wewe unavyoyajua
 
Unadhani share zinauzwa tu kibudu...tehteh

49% kwa majority shareholder mmoja tu

51% kwa members.....ambapo itakuwa by default hakuna haya ya subscriptions
Kwa taarifa yako tu: Katika hao wanachama mimi nimo tena niko siku nyingi tu na hakuna anayejua kuwa mimi ni wa_Kimataifa. Sitaki Simba ife bali iyumbe kwa kwenda mbele kila mwaka. Nikiwa ndani ya Simba nimejichanganya mithili ya sukari na chumvi, ili uitenganishe sukari na chumvi unahitaji mbinu za kikemikali kama paper chromatography kwa mchangayiko wa rangi. Kajifunze maana ya maneno hayo.

Yanga daima mbele mikia nyuma kila siku.
 
ulitaka afanyeje kama MO

Ulitaka aingie k wenye siasa za kipuuzi za simba

then utofauti wake ungekuwa ipi

tuipende ku shift blame kwa watu w engine katika Makosa yetu wenyewe
He is already behind it... stop pretending kama vile hahusiki kabisa

Hivi nyie mnadhani watu hawajui his reaction baada ya kukataliwa kuinunua in the first place

People are not idiots
 
Mkuu nyie mna mafanikio sana

Tuache Na Simba yetu

Endelea na Yanga Yenu yenye mafanikio kedekede

Tunayajua matatizo yetu kuliko wewe unavyoyajua

Kama mnayajua hayo matatizo yenu msije humu kulia lia basi. Kichwa cha hii threads mdau anaonyesha kachoka na anataka Simba iuzwe hiyo pekee ina maanisha mna matatizo lukuki na hamna wa kuwasaidia.

Sisi kama watani wenu wa jadi na Pia kwa kuwa Simba ni tawi la Yanga (rejea historia) hatuwezi kuwaona mnaangamia bila kuwaokoa.
 
Goodwill ya Simba..na jengo ndio 20 Billion wakati jengo tuu ndio gharama yake tafuteni viongozi bora tuu waiinue Simba..Mbona ilikua ni Timu nzuri kabla toka imepenyezwa rupia ya kuhujumu timu ili hii filimbi yenu ya iuzwe ionekana ina nguvu Simba au Yanga ni za wananchi akitaka timu anunue vitimu vidogo huko hata kwa milion 500 atapata...
wacha jengo kuna uwanja unaohitaji kuendelezwa kuna mauzo ya jezi ambayo yanaishia mifukoni mwa wachache timu yetu inahitaji viongozi bora na wanachama wenye uchungu na timu
 
mfumo wa team za ulaya unaeleweka na watu wana share pale kwa hiyo timu ikiuzwa umiliki wa timu unabadilika na utawala pia na unakua bora...huyo anaetaka kuinunua simba si nae atakua na maslahi na wachache tuu..

Isanga family umenena vizuri sana.
Wanachama watapata share timu ikiuzwa.
Kila mwanachama atapata alicho toa kuiboresha Simba.
 
Kama mnayajua hayo matatizo yenu msije humu kulia lia basi. Kichwa cha hii threads mdau anaonyesha kachoka na anataka Simba iuzwe hiyo pekee ina maanisha mna matatizo lukuki na hamna wa kuwasaidia.

Sisi kama watani wenu wa jadi na Pia kwa kuwa Simba ni tawi la Yanga (rejea historia) hatuwezi kuwaona mnaangamia bila kuwaokoa.

kwani jukwaa hili ni la mashabiki wa Yanga pekee mkuu

Tunaweza kuyajadili matatizo yetu sisi mkuu

Hatutaki manafiki kama nyie msiojitambua

Yanga haiwezi kuona kwa misingi Ipi...wakati matatizo yenu ni makubwa mara milioni kuliko simba
 
Tatizo lako wewe unaa element za kipumbavu. Tangu post yako ya kwanza inaonyesha dhahiri uko humu kwa ajili ya ku provoke watu na kuwatafutia Ban. Jukwaa la Michezo wastaarabu wanajulikana na wajinga wanajulikana tumeshaazoea humu kubadilishana mawazo na wanachama wa simba ila sio vilaza kama wewe . So next tym kama unaona huna mawazo constructive zaidi ya huu upuuzi unaoleta usi quote my Post. oh ukiona umeshindwa kujizuia just nitupie kwenye ignore list
 
Mpuuzi kweli wewe...who cares of looseholes of your like....pheeeeew...nicooncop
 
hivi huyu mo hahusiki na kufungwafungwa mi siwaaminigi watu hawa
 
Mpuuzi kweli wewe...who cares of looseholes of your like....pheeeeew...nicooncop

Halafu next time utukane kiswahili maana hayo matusi ya kuazima huyawezi. Au fanya umekosea unitukane tena coz hiyo nicooncop hakunaga kwenye dictionary ipo nincompoop tu.
 
Tuvimiliane ndg zangu!!!
7ba9cc3ec50c63c1fb1c598179ab7e83.jpg
 
Back
Top Bottom