Simba SC, klabu iliyozaliwa na Yanga SC

Hata Stefano hakuamini hadi alipomwona Yesu na kugusa ubavu wake ndipo akaamini kuwa alikuwa amefufuka. Wewe subiri siku ya kiama ukipenya na kufanikiwa kukutana na Karume utaamini.
Hivi Stefano kiswahili chake ndo Tomaso au Tomaso kiswahili chake ndo Stefano?
 
nipe source ya kuaminika!

kwahiyo inaonyesha upinzani wao umenzia baada wengine kusaliti na kujitoa?au upinzani wa jadi ulikuja kutokea baadaye sana

Kwa hiyo mama Karume, ambaye mumewe ndiye aliyewajengea Simba lile jengo lao na kuwapa jina la Simba badala ya Sunderland sio source ya kuaminika? Basi kamuulize Rage ndugu
 
nipe source ya kuaminika!

kwahiyo inaonyesha upinzani wao umenzia baada wengine kusaliti na kujitoa?au upinzani wa jadi ulikuja kutokea baadaye sana

Wasikilize Simba wenzako wanabwabwaja nini;


SOURCE: http://www.shaffihdauda.com/2012/10/dar-pacha-kuisimamisha-tanzania-kwa.html?m=1

Kwa hiyo unaweza kuona kabisa kuwa Simba ni ubavu wa Yanga, just like Adam and Eve. Lol!
 

Utukuzwe Ee Mungu wa pekee na wa kweli unayesikia na kujibu dua za watumishi wako. Leo imedhihirika kuwa uliwako, uko na utayekuja kwa kuwapa ushindi KCC kama mimi mtumishi wako Makoye Matale nilivyokuomba kwa unyenyekevu na kicho kikuu. Tangu sasa wakuu wajue katika jukwaa hili wewe unao uwezo wa kumwinua yeyote utakaye na kumdhiri yeyote anayejinuua kama klabu ya Simba. Hakuna shaka wewe ndiye Mungu wa kweli unayestahili kuabudiwa. Endelea kuibariki klabu yako uipendayo ya Yanga Afrika, huko waliko wafanikiwe sana na watakaporudi waendelee kugawa dozi kama ambavyo umekuwa ukiwabariki. Heshima, utukufu na nguvu ni vyako milele na milele, amina.
 
Last edited by a moderator:
...kusema dua ya kinafiki na iliyojaa uzindaki wa namna hii Mungu kamwe hawezi kuipokea usijidanganye, kilichotokea tayari kilikuwa kwenye mipango ya Mungu si katika mipango yako kama ujiaminishavyo.

unaambiwa usi-hukumu nawe ukaja kuhukumiwa.......sasa wewe unapoanza kuihukumu Simba ili hali unajiita Mtumishi unaabudu Mungu yupi???, na kipindi kile mnapigwa 5-0 na 3-1 hizo dua zilikua wapi????
 
Last edited by a moderator:

Hizi historia za kusadikika msiwe unatuwekea humu!!.... Inamaana Watanganyika hawakuwa na club za mpira... Kama ndiyo hivyo inamaana hata YANGA ni tawi la YANGA ya Zanzibar iliyoanzishwa na karume kwa hiyo African Sports za Dar na Tanga zilikuwa matawi... Kama ilivyo Celtic ya Ulaya na Celtic ya Afrika Kusini....

Hii historia yenu haiko realistic... mwandishi kachimbe tena
 

Ha ha hah! Hiyo ni kwa mujibu wa Mzee Kilomoni. Kwani unadhani asili ya mpira ni Tanganyika? Karume kaanzisha African Sport Zanzibar, akasaidia kuanzisha African Sports Tanga akasaidia kuanzisha Young Africans Sports Club DSM. Wazee wa migogoro baadaye wakajitenga na kuanzisha Simba (kama ilivyokuwa kwa Pan Africans). Hivyo simba ni tawi la Yanga upende usipende. Haya na wewe lete historia yako sasa.
 
unatumia mfano mbaya

Mkuu ni maneno ya mzee Saidi Kilomoni hayo. Simba ilianzishwa toka ubavuni mwa Yanga. Usijisikie mnyonge mkuu, ndio hali halisi hiyo.
 

I salute you Great Thinker, KCC kashafanya yake kama ulivyotabiri.
 
Last edited by a moderator:

Hujambo Mkuu. Kasome Ebr. 11.
 
Ni Tomaso, nilikosea Mkuu Masuke, siyo Stefano: niwieni radhi wote mliokwazwa na posti hii.

Mkuu si unajua sisi kule kwetu Simiyu tunatumia biblia ya kisukuma sasa ndo maana nikataka nijue labda kwa Kiswahili jina la Tomaso ndo huitwa Stefano. mhala sana omayu?
 

Mkuu Simba haikuundwa kutoka Yanga sema iliundwa na wachezaji/viongozi waliokuwa Yanga baada ya kuona hawaendani na falsafa ya Yanga kwa hiyo haiwezi kuwa tawi la Yanga, ingekuwa ni tawi endapo falsafa zao zingekuwa zinaendana lakini sasa Yanga na Simba ni vitu viwili tofauti kabisa.

Unachotaka kusema ni sawa na kusema kwamba chama cha Republican cha Marekani ni tawi la chama cha Democratic kwa sababu tu wanachama wengi wa Democratic ndo waliounda chama cha Republican.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…