Simba SC, klabu iliyozaliwa na Yanga SC


Kwa hiyo unakubali kuwa Simba imetokana na Yanga?
 
Kwa hiyo unakubali kuwa Simba imetokana na Yanga?

Mkuu hapa tutabishana mpaka basi, Wazo la kuanzisha Simba lingetolewa na kamati ya Utendaji wa Yanga tungesema imetokana na Yanga lakini sasa kamati ya utendaji haikuwa na wazo la kuanzisha timu nyingine kutokana na timu iliyokuwepo, kuwa na wachezaji na baadhi ya watu waliokuwa Yanga na kwenda Simba haimanishi kwamba imeanzishwa kutokana na Yanga.

Kiutani wa jadi tunaweza kusema hivyo kama sahivi tunavyosema kwamba Yanga ni sawa na Simba Veterani kwa sababu tu baadhi ya wachezaji walishawahi kuchezea Simba, (Juma Kaseja, Ally Mustafa, Deo Munishi, Emmanuel Okwi, Mrisho Ngasa, Athumani Idd, Kelvin Yondani), kama utakubaliana na hiyo dhana kwamba Simba ilitokana na Yanga basi inabidi ukubali pia kwamba Yanga ya sasa ni Simba Veterani.
 

Huoni aibu kumjumuisha Ngassa?
 
Huoni aibu kumjumuisha Ngassa?

Mkuu kabla ya kuandika hii sentensi yako umesoma vizuri nilichokiandika lakini? nimesema waliowahi kuchezea Simba. kwa hiyo unataka kuniambia Ngasa hajawahi kuchezea Simba?
 

Ndugu, sioni hata unachobisha ni nini hasa. Unakubali kuwa mgogoro ndani ya klabu ya Yanga ndio uliopelekea baadhi ya wanachama na wachezaji wa Yanga kuamua kujitenga na kuanzisha timu ya Simba. Halafu unakataa kwamba klabu ya Simba haikutokana na Yanga. Huoni kuwa bila mgogoro ndani ya Yanga huenda kusingekuwa na Simba leo hii? Kwamba Simba haikuanzishwa kwa wazo huru bali ni wanayanga walioamua kuasi? Hii inatofauti gani ni iliyokuwa Pan Africa?

Kuhusu Yanga kuwa Simba veteran ni mtazamo wako tu. Ngasa si veteran na hajaanzia Simba. Yondani amechukuliwa akiwa kijana mbichi kabisa, Okwi sijui kama Simba walimwacha kwa umri, au amesajiliwa toka Simba. Ninavyofahamu mimi Okwi kasajiliwa toja Villa ya Uganda na si Simba veteran. Dida katoka Azam, labda kama nimekosea, tena hajaanzia mpira Simba. Hali kadhalika Barthez alitupiwa virago kabla Yanga haijamwokota ili kunusuru kipaji chake, kama ilivyokuwa kwa Nurdin. Kaseja naye katoswa kwa uwezo si umri, makipa si kama wachezaji wa kati. Sasa sijui unatumia mazingira yapi kusema Yanga ni Simba veterani. Waliosajiliwa toka Simba hapo ni Yondani na Mrisho pekee.

Hao unaowaita maveterani asilimia kubwa ni tegemeo kwenye timu zao za taifa.

Lakini Simba imeanzishwa na waliokuwa wanachama damu wa Yanga, huo ni ukweli mchungu. Lazima muumeze tu.
 
tatizo liko wapi hata liverpool ilitoka kwa everton na leo liver ni successfull kuliko everton
 

Mkuu hoja yako kubwa ilikuwa ni kwamba Simba ni tawi la Yanga na mimi nikakwambia sio tawi la Yanga kwa sababu haikuwa wazo la uongozi kuwa na timu nyingine na ukizingatia kwamba Yanga ilikuwa na mwaka mmoja tu kipindi hicho hivyo sidhani kwamba watu wote waliokuwa Yanga walikuwa na mapenzi na Yanga labda walikuwa Yanga tu kwa sababu hapakuwa na chaguo lingine na ndo maana ilichukuwa mwaka mmoja tu kuanzisha timu nyingine.

Jirani yako akiwa anaweka vifaa vya ujenzi kwako wakati wa ujenzi haina maana kwamba nyumba ikikamilika utasema kwamba nyumba ile imetokana na nyumba yako simply tu vifaa vya ujenzi vilikuwa vinahifadhiwa kwako.

Kama umenisoma vizuri sijasema wachezaji walianzia Simba au kusajiliwa wakitokea Simba, nilichosema waliwahi kuchezea Simba na hiyo kuita Simba Veterani ni dhana tu ambayo inatokana na utani wa jadi kama wewe unavyotaka kutuaminisha kwamba Simba imetokana na Yanga ndo maana nikakwambia kama unakubali dhana hiyo basi kubali pia kwamba Yanga ni Simba Veterani maana si ina wachezaji saba waliwahi kucheza Simba au ni uongo?
 

Si kweli kwamba hoja yangu ni kwamba Simba ni tawi la Yanga. Mimi nasema Simba imetoka ubavuni mwa Yanga, kama Adam na Eva. Eva hakuzaliwa na Adam bali alichomolewa ubavuni mwake. Wakawa viumbe wawili tofauti, ingawa Adam akapewa ubosi.

Kuhusu nyumba, usiongelee vifaa kuhifadhiwa, bali ongelea watoto wa kike. Mtoto wa kike anapoolewa huenda kutengeneza ukoo wa upande wa mwanaume. Ndio maana hata jina lake l ukoo hubadilika, kama ilivyo kwa Simba. Wale walikuwa wanachama halali kabisa wa Yanga. Watoto waliozaliwa ndani ya klabu ya Yanga, familia ya Yanga. Yanga imezaa watoto wanne halali kabisa kama ifuatavyo;

African Sports - Tanga - dume
Toto Africans - Mwanza - dume
Pan Africans - Dsm -dume
Sunderland - Dsm -jike

Sasa hayo matoto madume yoote humkumbuka mzazi kwa vile ni ukoo mmoja, lakini huyo malkia yeye amekwenda kuendeleza ukoo mwingine kabisa na ndio maana kabadili hata ubin wake kumfuata ukoo wa mume. Sie tunachofanya ni kukutakieni maisha mema na yenye mafanikio. Hamna urithi huku kwetu labda tusubiri katiba mpya tuone itakuwaje.

Poleni sana, lakini huo ndio ukweli.
 

Kwa kweli utani wa jadi ni balaa, habari uliyonukuu inasema wazi kabisa klabu ya kwanza kabisa ni African Sports Club ya Zanzibar na ndo baadaye hizo zingine zikafuatia, kwa nini sasa usiseme vilabu vyote hivyo baba yao ni African Sports Club ambaye alishafariki kutokana na uzee na waliobaki sasa ni watoto including Yanga mtoto mkubwa ambaye anakaribia kufa.

Mkuu inaonekana huna taarifa kabisa kama kuna Patronial na Matronial society, kawaulize waluguru watakwambia kama mtoto wao wa kike huenda kuendeleza ukoo mwingine.
 


Kwani Simba ni waluguru?

Mkuu African Sports ya Zenji ilianzishwa sambamba na Yanga, sio kwamba Yanga iliundwa na wanachama wa African Sports.

Pia mwanzilishi wa African Sports aliendelea kuwa mwanachama mwaminifu ya Yanga mpaka mauti.

Hawa wengineo (Toto, AS, Pan) walitokana na Yanga, sio sambamba na Yanga. Simba yeye alikuwa home girl mpaka alipoolewa ukoo wa Sunderland. Lakini asili yake ni Jangwani, mwee!
 
Kwa hiyo mama Karume, ambaye mumewe ndiye aliyewajengea Simba lile jengo lao na kuwapa jina la Simba badala ya Sunderland sio source ya kuaminika? Basi kamuulize Rage ndugu

Karume hakujenga jengo la Simba, alitoa msaada tu wa fedha, labda kwa jengo la Yanga ndo alijenga, soma hapa chini.
 

Nimekutajia waluguru kama mojawapo ya jamii inayofuata matronial. Haya bana Simba alienda kuanzisha ukoo mwingine ambao ulikuja kuwa na vijana shupavu wakaja kutoa vipondo kwa ukoo wa babu yao kama ifuatavyo.

Awamu ya Nyerere 6-0, Awamu ya Mwinyi 4 -1, awamu ya mkapa 4-1 na awamu ya Kikw ete 5-0; naona uchaguzi wa kuleta awamu nyingine unakaribia hil i ukoo mwingine ambao Simba alienda kuuendeleza uweke rekodi nyingine.
 

Awamu ya Shein: Mapinduzi Cup-kapa!
 

Yeah, binti Simba kaolewa. Siye ni kumtakia maisha mema. Ubavu wa Yanga kagongwa talaka kaondoka zake. Bila Yanga no Simba, fact!
 
Yanga hatukuogopa kushiriki isipokuwa Simba wasio na akili kama Wagalatia wanadhani kwamba eti tuliogopa kushiriki. Kwa Simba mapinduzi ni nafasi yao ya mwisho, Yanga tuna majukumu ya CECAFA na CAF.

Tnx
Private Members Club Insurance
 
Awamu ya mtani jembe, Yanga akakimbia kushiriki mapinduzi cup.

Mkuu Masuke ni afadhali kutofanya mtihani; kuliko kufanya mtihani na kupata ziro (beseni, yai, karai n.k: KCC 1-0 Simba).
 
Last edited by a moderator:
Ukiwaambia Yanga timu yenu ya Kizanzibara watakataa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…