Simba SC kucheza na Power Dynamos Agosti 6, 2023 kwenye kilele cha Simba Day

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Ahmed Ally amesema Siku ya Simba Day wataalika Mabingwa wa Zambia, Power Dynamos kwenye kilele cha siku ya Simba Day.

Wasanii wengi wakubwa watakuwepo.

Rekodi ya mwaka jana walijaza uwanja saa 7 mchana, mwaka huu wanataka kujaza uwanja saa 6 mchana.

Kwa mujibu wa Ahmed Ally, Simba SC inajali sana wanachama na mashabiki wao hivyo wameweka viingilio rafiki.

Kiingilio cha chini kabisa kitakuwa Tsh. 5000/- kwa mzunguko.

Aidha, waliohusika kupandisha kibegi kwenye kilele cha mlima kilimanjaro wataalikwa kwenye kilele cha siku hiyo na kitambulishwa rasmi, na Simba itagharamia huduma zote zinazowahusu kuanzia safari yao.
 
Wanasimba mkaujaze uwanja wa mkapa.
Tamasha lenu likafane.
Eti ooooh tamasha lao limedoda uwanja haujajaa.
Rekodi ya kuujaza uwanja wa mkapa saa saba inashikiliwa na simba.
Najua lote hili la daslam unaenda kujianika kwa mkapa.
Shida zote hizo za nini wakuu.


Tatizo simba inataka kuonekana ni kubwa kwa yanga kwa kuivizia yaani wanasubiri yanga wafanye matukio iliwao waangalie ni yapi yanga hajayafanya ili kuipiku.
Fanyeni vitu kwa maslahi yenu.



Mahesabu madogo tu ya akili
Mzunguko
40000*5000= 200000000 (simba)
30000*10000=300000000 (yanga)

Uwanja utajaa ila hamna manufaa.
 
Manufaa kwa Simba ni wanachama na wapenzi kushiriki kwenye siku yao na kwa ajili ya maokoto ya pesa ya kulipa madeni ya usajili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…