Deo Corleone
JF-Expert Member
- Jun 29, 2011
- 17,006
- 13,281
Majanga juu ya majanga.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ha! Unasemaje? Hatuhusika na wa mchangani sie.itakuwa yanga hawa wamesababisha
Historia tu hiyo, yeshapita.Simba ukawa bado tumo wewe, mnyama for life, ndala goli 5-0 sijui watarudisha lini?
Acha hizo wewe. Pesa hiyo ni kidogo sana kwetu.Jamani Simba hadi wanatia huruma,sasa wakishuka daraja hata ndondo cup si wataikosa?
[emoji134] [emoji134] [emoji134]
Maana sioni namna wanayoweza kulipa hizo pesa.
Labda wapitishe bakuli. [emoji6]
Mishahara yenyewe wachezaji mnawalipa tarehe 73Acha hizo wewe. Pesa hiyo ni kidogo sana kwetu.
Pesa za okwi zinawapa kiburi eeh?Acha hizo wewe. Pesa hiyo ni kidogo sana kwetu.
TFF ikizuiwa kushiriki kimataifa maana yake ni nini?LATEST: Simba imepewa amri na FIFA kuhakikisha inalipa deni la Sh64milioni za Mkenya Donald Mosoti ndani ya siku 30 kuanzia leo, vinginevyo itapokonywa pointi na kushushwa daraja.
TFF nayo ikishindwa kusimamia amri hiyo inafungiwa kushiriki michuano ya kimataifa.
Walifurahia kuyachota Mamilioni ya Etoel du Sahel sasa kibao chawageukia wao.
====================
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limeipiga faini ya Franc 2,000 za Uswisi (sawa na Sh 4,582,000 za Tanzania), Klabu ya Simba baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupuuza maagizo ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Chamber) ya shirikisho hilo.
Kamati ya idara hiyo iliyokutana na Aprili 20, 2016 huko Zurich, Uswis ilitumia Franc 500 (sawa na Sh 1,145,500) hivyo Simba pia imeagizwa kuzilipa ikiwa ni gharama za kikao cha kufuatilia utekelezaji sakata la mchezaji huyo, raia wa Kenya.
Simba imeelezwa kupuuza kumlipa mchezaji Donald Musoti Omanua kwa wakati tangu mkataba wake uvunjwe. Musoto aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa alilalamika FIFA ambayo iliona ana hoja na hivyo Simba kutakiwa kumlipa dola 29,250 (sawa na Sh 62.8 milioni) na kiasi kingine anachodai ni Dola 600 (Sh 1,290,000) zilizobaki katika usajili ambapo jumla yake ni Sh 64.2 milioni. Pia Mosoti anamlipa Mwanasheria wake dola 2,000 (Sh 4.3 milioni) kwa ajili ya kusimamia kesi hiyo.
Felix Majani, Mwanasheria wa Musoti, ambaye pia ni mmoja wa wanasheria wa FIFA, alifungua kesi katika shirikisho hilo kuwashitaki Simba kwa kukiuka makubaliano ya mkataba na mteja wake.
Kwa kosa hilo Simba inatakiwa kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016. TFF imekuwa nakala na maagizo kuisimamia Simba inalipa kiasi hicho cha fedha.
Simba imeagizwa kulipa stahiki zote za Mosoti ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kupokea barua hiyo ya FIFA iliyoandikwa Mei 3, mwaka huu na kufika Tanzania leo Mei 6, 2016.
Katika barua hiyo ambayo TFF ina nakala yake, Simba imepewa amri ya kuhakikisha inalipa na isipotekeleza agizo hilo mara moja itakatwa pointi tatu katika mechi zake Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara –VPL.
FIFA imekwenda mbali zaidi ikisema ikiwa klabu hiyo kama haitalipa katika muda uliopangwa yaani siku 30 kutoka sasa, FIFA itaishusha Simba daraja kutoka Ligi Kuu Tanzania Bara hadi Ligi Daraja la Kwanza au zaidi.
Kwa upande wake, TFF imagizwa kuhakikisha uamuzi huo unasimamiwa vema utekelezwaji wa maagizo hayo vinginevyo itachukuliwa hatua stahiki ikiwamo kuiondoa Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
Mkuu GENTAMYCINE ameacha kuishabikia Simba, Mkuu sembo haonekani humu jukwaani. Nadhani kwa taarifa hii kuna member mwingine kesho nae atatangaza kuhama timu.
Tuko busy tunapambana na wanaoficha sukari, mambo ya Simba tumepumzika kidogo.
hii itawafaa zaidi.....Waombe mkopo kwa ndugu zao Azam watapewa