Simba SC: Kwanini tusibebe CAF Champions League?

Simba SC: Kwanini tusibebe CAF Champions League?

Mtanisamehe wana simba....


Wydad Casablanca my favourite team..

Wydad Casablanca or Al ahly, kati yao anaondoka na ndoo mazima...



Wydad oyeee 🔥🔥🔥
 
1. Sisi wana Simba tumefurahi kwa kuwa team inayoongoza kundi gumu na kupata matokeo mazuri kuliko team yoyote iliyovuka robo fainali.

2. Ukweli ni kuwa team tishio kwa Simba kutofika final ni Al Ahly pekee sababu team hii ikifika semi final huwa inabadilika na inakua na njaa zaidi ya kombe kuliko team yoyote itayovuka robo fainali.

3. Ombi kwa Mamelod Sundown watusaidie kuwatoa Al Ahly kwenye hatua ya Robo fainali kwa sababu Sisi Simba Sc tuta deal na CR Beloizdad na kuwalipia kisasi ndugu zetu wakenya Gor Mahia.

4. Najua lengo mama la club yetu sasa ni kuchukua ubingwa wa Africa ila tunaogopa kuweka wazi hilo kwa sababu ya kuondoa maneno ya husda na kupata sehem ya kujitetea lakin club vigogo tumezitetemesha na zinatuogopa kwa sasa.

5. Nakumbusha Simba kupitia msemaji wetu manara kwa sasa muweke wazi lengo la kuchukua ubingwa wa Africa kwa sababu,kwa sasa tunayo nia,nguvu ,Sababu na hata uwezo.

6. Tumewahi kufika nusu fainali club bingwa Africa, Fainal shirikisho,Robo fainali ligi ya mabingwa na sasa tupo robo fainal nasema kutoka moyoni kwa miaka yote hii team tuliyonayo safari hii inaweza ikabeba kombe hili kuliko team yoyote iliyopita, maana yangu ni kua Spain ingeshindwa kubeba world cup 2010 sijui ni mwaka gani wangebeba sababu mwaka ule walikua wana kikosi bora kabisa katika historia yao kimpila.

7. Ni kazi kubwa imefanyika mpaka Simba kufika robo fainal ,nasisitiza ni kazi kubwa isiyoweza kutafsiriwa kwa lugha rahisi sasa ni bora tukamalizia kazi kwa kufikiria kuubeba ubingwa sababu kila ukiitazama simba kwa jicho la ziada unaona kabisa hili linawezekana

8. Simba ni bora sana kwa sasa Africa, kama ukiangalia jinsi tumecheza na Al Ahly, Al Merreikh, As vita, Plateau United, Platinum wapinzan wote hao tuliwaacha mbali sana kimchezo kiasi kwamba walikua hawaelewi wanafanya nin uwanjani na wote walikubali kua tumewazidi kimchezo, Hili linafanya team zilizobaki kutuogopa na kuwaza watafanyaje wakikutana na sisi.

9. Uwanja wa mkapa ni miongoni mwa viwanja vinavyoogopwa kwa sasa Africa hasa kikitumiwa na Simba hii ni Advantage sana kwetu na nashukuru wachezaji na benchi la ufundi wanajua hili na wapo well organized.

10. Ni ushindi kwetu hata tukiishia robo fainali na nachukua nafasi hii kushukuru na kuipongeza team na hatutawalaum tukiishia Hapa, lakin nna uhakika tukisema tubebe kombe hili hakika tutaweza.
Ndo mipango yetu hiyo
 
Hamna huo uwezo ....

Narudia tena uwezo Hamna...



Nasema hivi simba hana uwezo huo kenge wewe
Sasa mbna umesisitiza vizuri na unanitukana juu



Sinaga kauli mbovu tusitukanane kutaftiana BAN sababu wengine tukifungua midomo tuna kauli chafu



Anyway najua una hasira na matokeo ya Yanga na matokeo ya simba yanakuumiza zaidi , , ,ko samahan kwa niaba
 
SImba ubingwa mchukue nyie underdog? Tarehe 9/4 al ahl anawapiga mkono na kusambaratisha ndoto zenu za alnacha
Al ahly hawezi kumfunga simba msimu huu,iwe away kwake Cairo.Hiyo match itatuma salam mbaya sana kwa vilabu vingine vinavyoshiriki kombe hilo.
 
Back
Top Bottom