Mnyuke Jr
JF-Expert Member
- Jul 3, 2021
- 4,472
- 6,391
Wasalaaaam wakuu
Mimi ni mdau na shabiki wa Yanga mkubwa sana ila kwa ndoto nilizopata usiku wa kuamkia leo ni taswira halisi ya kitakacho enda kutokea huko Kigoma katika fainali ya kombe la shirikisho Tanzania baina ya mahasimu wakubwa na watani jadi Yanga na Simba
Ndoto ya kwanza nilianza kuota Nikiwa kibanda umiza na katikati wa watu wakiwa wanashangilia sana ubingwa wa simba, nilifadhaika sana ndani ya nafsi yangu kwa mimi ni shabiki na mpenzi wa Yanga na nilitamani timu yangu iweze kushinda mchezo huo, ila ghafla nilishtuka kutoka usingizi na nikiwa na wenge kwa kilichotokea kwenye ndoto na nikamshukuru Mungu lile halikuwa tukio halisi.
Baada ya kupitiwa na usingizi, tena kwa mara ya pili nilianza kupata ndoto ya mchezo huo ambapo mchezo hadi dakika ya 90 zinamalizika hakuna timu iliyo ona lango la mwenzake na hivyo mchezo kuelekea kwenye hatua za penati(Matuta) na mwisho Simba akainuka tena bingwa wa mashindano hayo kwa ushindi wa penati wa Simba 5 na Yanga 3, ila nikashtuka tena kutoka usingizi na kutambua nilikuwa katika njozi tu na sio uhalisia wa kilichotokea
Ila ndoto zinanipa mashaka kwani nimekuwa ni mtu ambaye huwa napata njozi za namna hii mara kwa mara, hasa za kwenye mechi za mpira wa miguu na Zimekuwa zikitokea kama nilivyopata ndoto na kupelekea hata hii ndoto niliyopata usiku wa kuamkia leo ni kweli simba atakuwa Bingwa katika mashindano hayo
Hii ni fursa kwa watu wa betting katika mechi hii, unaweza kubet kwa option mbili ya kwanza kumpa simba ubingwa na ya pili ni kumpa simba ubingwa tena kwa njia ya penati na hakika utaweza kushinda katika betting yako
Mwisho nakupongeza sana Mtani kwa ubingwa huu wa Kombe la shirisho Tanzania kwa mara ya pili mfululizo.
Ahsante.