Simba SC Mkitaka Kuwa Mabingwa Msimu Huu Mfukuzeni Pablo, Mpeni timu Matola

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
MKITAKA UBINGWA FANYENI HIVI.

Nimesikia mazungumzo kibao kuhusu Matarajio ya Simba SC kutwaa ndoo msimu huu. Cha kushangaza zaidi hakuna anaye fahamu nini kifanyike ili muwe tishio katika mbio za Ubingwa wa msimu 2021/22.

Ushauri wangu kwenu ni kumtawaza Selemani MATOLA awe Kocha mkuu wa klabu au Kumfukuza mapema iwezekanavyo kabla hamjachelewa.

WHY?

Selemani MATOLA ndiyo mwenye kuongoza hujuma, figisu na chokochoko dhidi ya Timu akiwa na lengo kuu la kuhakikisha matokeo mabaya yanapatikana ili yapelekee kufukuzwa kwa Pablo.

Njama zake ni za siri mno hata baadhi ya viongozi wenu hawana uwezo wa kuamini hilo.

Tamaa yake kubwa ni kuweka Ufalme wake katika nafasi ya ukocha katika Klabu yenu. Baada ya kuona nafasi hiyo ni ngumu kuipata kiurahisi, sasa anapanga kuuonyesha Uongozi wenu kuwa makocha wazungu (Aussems, Da rosa, na Pablo) hawana uwezo wa kuifikisha mbali klabu.

Bila kujua. Hizo figisu zake zinashusha morali ya utendaji wa wachezaji haswa wale wazawa.

Hakikisheni mnampa timu haraka sana, kama itashindikana mfukuzeni kabisa kwenye benchi ufundi.

Narudia tena.

"Matumaini yenu ya ubingwa wa msimu huu yako katika kilindi cha Moyo wake ulio jawa na tamaa za kutaka kuwa Kocha mkuu wa Simba"

FORM ALIYONAYO YANGA SC

Kwa Yanga SC hii iliyoko kwenye form, nina uhakika matokeo mabaya kwake ni sare tu. Hivyo itawapasa kutoa sare mechi 4 ili kufikiwa alama na SimbaSC. Na wakati huo huo Simba SC ina kibarua cha kushinda mechi zake zote.

Je kwa hali iliyo ndani ya bench la ufundi la SIMBA SC unadhani inawezekana? Si rahisi.

KUMBUKIZI
Nakumbuka niliwahi kuiandikia barua AZAM FC iliyotaka imuondoe Iddi CHECHE kwenye bench lao la ufundi. Jambo jema ni kwamba wakatii.

Tamaa ile ile aliyokuwa nayo Cheche, sasa imeamia kwa Matola.

Matola ataitafuna klabu yenu chini kwa chini mpaka mkija kushtua Mnakuta YANGA SC Katwaa ndoo za ligi mara 3 mfululizo.

-Asiye Sikia la Mkuu...
 
Naunga mkono hoja ila na ww kama uliweza kuwaandikia Azam barua ya kutia mchanga kibarua cha Cheche,kwa nn usifanye hivyo kwa Thimba ili wamtimue huyo Matola? Utakapoaandika hiyo barua usisahau tu kuonggeza fact 2. 1. Boko na Mugalu waachwe na 2. Wasajiri mfungaji wa maana kwa Maana ligi letu ni kubwa kwa sasa. Kila timu kwa sasa inawachezaji wa kuchezea Thimba ba Nyanga so lazima walione hili
 
Matola ana CV ya kuwa kocha mkuu? Tuanze hapo kwanza. Unapoleta maoni yako jaribu kutafakari sawa , Pablo afukuzwe then yeye awe kocha mkuu anazo sifa? Ausem mwenyewe tuu alikuwa anakaa benchi club bingwa sembuse huyu matola bado mwanafunzi [emoji1]
 
Matola ana CV ya kuwa kocha mkuu? Tuanze hapo kwanza. Unapoleta maoni yako jaribu kutafakari sawa , Pablo afukuzwe then yeye awe kocha mkuu anazo sifa? Ausem mwenyewe tuu alikuwa anakaa benchi club bingwa sembuse huyu matola bado mwanafunzi [emoji1]
Niko katika Circle ya ndani kabisa ya "Watu Wake".

Ninafahamu wazi kuwa ana sifa za kuiongoza Klabu Kwenye Ligi na sio Kwenye michuano mikubwa ya Africa.

Ujinga wa Kocha wenu msaidizi na tamaa zake bado anaona inafaa kupewa kijiti.
 
Nimekwisha fanya hivyo tangu Matola atoke masomoni morogoro.

Nadhani wameiweka kwenye dust bin.

Sina tija ya kuwaandikia tena.

Ninauhakika ifikapo May baada ya Mabingwa Wa Kihistoria Kukabidhiwa Taji watarudi kuisoma upya.
 
Matola uwezo wake ni mdogo sana,uswahili ndio unaombeba
Niko katika Circle ya ndani kabisa ya "Watu Wake".

Ninafahamu wazi kuwa ana sifa za kuiongoza Klabu Kwenye Ligi na sio Kwenye michuano mikubwa ya Africa.

Ujinga wa Kocha wenu msaidizi na tamaa zake bado anaona inafaa kupewa kijiti.
 
Ungesema au Kushauri Benchi zima la Ufundi kuanzia Kocha Mkuu Pablo Franco na Msaidizi wake Seleman Matola wako Wote wafukuzwe tungekuona una Akili ila kwa sasa tunakuona ni Kinyume chake.
 
Kinachoiponza Simba Ni kwamba viongozi Ni watu wanaooneana aibu.
Pia ushkaji umetamalaki hapo Simba.
Kwa club zinazojielewa Matola hakupaswa kuwepo Simba maana Ni mtu fulan anayegawa wachezaji kwa namna ya kiswahili Sana.
Watu kila siku washatoa tahadhari juu ya Matola lakin viongoz wanamwonea aibu na kumgwaya.
Na yeye ashajua Hilo kuwa hakuna wa kumfanya kitu,.
Fuatilia upangaji wa kikosi Cha Simba km una jicho la kimpira utajua Waz Matola Ni mweupe Sana kichwani au anafanya kusudi ili timu isue sue ,rejea hata sab anaforce Sana wachezaji fulan waingie bila kuangalia mchango wao utakua na faida.
Jana ndio nimechoka balaa kumwanzisha bocco na kagere alafu chama anakaa nje na viongoz wanaangalia tu huu uhuni.

Mimi Bado naamin Simba Ina wachezaji wazur Sana tu shida ipo kwenye benchi la ufundi .Futa wote leten banchi jipya ,ikiwezekana leteni kocha ambaye atakuja na kocha msaidiz wake na sio huyo matola ambaye Kaz yake Ni kuwaharibia makocha wa kigeni.

Narudia Tena ,nyie viongozi wa Simba fukuza Matola huyo ndie mchawi wenu hapo Simba.
 
Mtamuonea Matola bure. Mapungufu makubwa ya Simba sasa hivi ni mshambuliaji namba tisa mwenye hadhi ya kuchezea klabu kubwa kama Simba. Mugalu, Kagere na Boko wote viwango vyao vimeshuka ghafla. Kosa kubwa lilianzia kwenye usajili wa dirisha kubwa likaja likarudiwa tena kwenye dirisha dogo la kutosajili mshambuliaji wa kati. Hivi kwa krosi zile za jana kutoka kwa Sakho, Mohamed Hussein, Bwalya, Mwenda (jana kajitahidi kupiga krosi vizuri) na mipasi ya akina Chama, Kanoute na Mkude bado Kagere, Mugalu na Boko walishindwa kufunga halafu lawama anapewa Matola? Hapana aisee tazameni vizuri Simba inavyocheza mtaona kuanzia nyuma mpaka katikati hakuna shida kubwa lakini inapofika zamu ya kufunga washambuliaji hawatimizi wajibu wao.

Simba mwaka huu mtatupa lawama kwa kila mtu hata wasiohusika lakini mchawi wenu ni viongozi walioamini kuwa Mugalu, Kagere na Boko watawapa mataji. Kikubwa tu kwa benchi la ufundi wawekeze kwenye mbinu zao tu kulingana na adui watakayekutana naye iwe kwenye ligi au shirikisho kwa sababau washambuliaji wao ni hao hao hakuna namna ya kusajili wengine mpaka msimu uishe.
 
Sioni mchango wowote wa Matola kama kocha msaidizi wa Simba SC, anatakiwa afukuzwe haraka sana sambamba na kocha mkuu.
 
naam kama jamaa wenu alivyopitia mlango wa uwani kudhamini ligi
Kajitoa siku naona kelele za GSM zimepungua, zimebaki za miamala,nawakumbusha kwa hali mnayoenda nayo ya mbeleko andaeni fungu na kwenye shirikisho CAF.
 
Wote wawili hakuna mwenye uwezo wa kuipa Simba Ubingwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…