Simba SC na AS Vita: Tushangilie kimoyomoyo baada ya tamko la Polisi?

Simba SC na AS Vita: Tushangilie kimoyomoyo baada ya tamko la Polisi?

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Simba SC na AS Vita ya DRC Kesho 03.04.2021 saa 10 jioni

Ifikapo kesho saa 10 jioni pale uwanja mkubwa wa soka Tanzania maarufu kwa Mkapa kutakuwa na mtanange wa kukata na shoka kati ya wawakilishi wa Tanzania ligi ya Mabingwa Simba SC na AS Vita ya DRC.

CAF imeruhusu mashabiki 10,000 kuingia uwanjani. Hawa ni watu wengi sana kukaa sehemu moja na wanatosha kuipa hamasa timu mwakilishi wetu. Lakini kumbukeni kuna zuio la Polisi kuhusu shamrashamra. Je, Simba wakifunga kesho tukae kimya? Tushangilie kimoyomoyo?

Polisi tunaomba ufafanuzi tusije ishia mahabusi watu 10000.
 
Shamra shamra ni tofauti na kushangilia! Kushangilia ni kuitia hamasa timu wakati inacheza bila kujali inacheza vizuri au vibaya. Shamra shamra ni kufurahia ushindi. Pendekezo: Baada ya kipenga cha mwisho kusiwe na shamra shamra zozote hata kama simba itashinda kama tunavyotarajia. Tutoke uwanjani kama tunatoka kwenye msiba ! Lakini kushangilia wakati timu inapocheza hiyo ni Kazi kama zilivyo Kazi zingine. Kila mtu anajua kuwa kila siku Kazi zinaendelea pamoja na kuwa tupo kwenye maombolezo!!
 
Nawewe nae!!
kwaiyo kesho Simba wakicheza mashabiki watakua wanafanya shamrashamra au wanashangilia?
 
Back
Top Bottom