Simba SC na Dar Young Africans zilipishwe kodi kama wengine

Simba SC na Dar Young Africans zilipishwe kodi kama wengine

Mars 12

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2021
Posts
221
Reaction score
349
Najua wengi wataudhika lakini wizara ya fedha chini yabkijana shupavu Waziri Mwigulu Nchemba wawawekee timu hizi 2 utaratibu wa kulipa kodi kama makampuni,mashirika,viwanda n.k kodi haibagui.

Kodi sio hiyari ni lazima.Simba na Yanga waajiri wahasibu kama makampuni mengine na wautangazie umma faida au hasara kabla ya kodi.
Waziri Mwigulu timu zote duniani za michezo hasa mpira wa miguu zinalipa kodi.Mfano tu Arsenal walitoa statement ya mahesabu yao kuonyesha walipata hasara ya paundi milioni52 kabla ya kodi.

Hii inamaanisha kuwaambia wapenzi na wanachama wao hali ya kifedha klabuni lakini bado wakazungumzia kodi. Wizara husika haina budi kuwataka simba na yanga waweke mahesabu yao kila mwaka,wawasilishe wizarani na wakadiriwe kama wengine kiasi cha kodi wanachotakiwa kulipa.Waziri Nchemba kodi haichagui.Nawasilisha.
 
Zikiwa kampuni zitalipa kodi ya mapato, ila kwa sasa wanalipa SDL, PAYE
 
Kwa nini iwe kwa Yanga na Simba pekee! Badala ya Vilabu vyote vya michezo!
 
Naona msumari umeingia kwenyewe. Bado idara ya maji inataka kuongeza km 2000 hivi.
Weka
Umeme
Miamala
Visimbusi
Maji
Kupanda kwa vifurushi inatakiwa 100mb tununue kwa 10,000
Hapo tutakuwa tunaona watu wengi wanaongea peke yao
 
Back
Top Bottom