Simba SC na Timu zingine 7 Kutocheza hatua za Awali CAFCL bali zitaingia Makundi Moja kwa Moja

Simba SC na Timu zingine 7 Kutocheza hatua za Awali CAFCL bali zitaingia Makundi Moja kwa Moja

Wakati Timu Moja mbovu mbovu nchini Tanzania na isiyo na Uzoefu wa Kucheza CAFCL japo ilibahatisha kufanya vyema CAFCC ikianza Kucheza Mechi zake Mbili au Nne za Hatua za Awali ambapo GENTAMIYCINE nina uhakika itatolewa na kurejea Kucheza NBC Premier League CAF wametoa Utaratibu mpya ambao unaihusu Timu bora Tanzania na Afrika ya Simba SC.

Taarifa rasmi ikufikie kuwa CAF wameamua Timu Nane ( 8 ) za Barani Afrika ambazo zitacheza Michuano mipya ya SUPER CUP hazitacheza tena Hatua za Awali za Michuano ya CAFCL bali zitaingizwa moja kwa moja katika Makundi na kuanzia huko.

Timu zenyewe ni hizi zifuatazo......

1. Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
2. Al Ahly (Misri)
3. Wydad Casablanca (Morocco)
4. Esperance du Tunis (Tunisia)
5. Simba SC (Tanzania)
6. TP Mazembe (Congo DR)
7. Petro du Luanda (Angola)
8. Enyimba (Nigeria)

Chanzo: Mitandao Mikubwa ya Michezo Afrika

Mkiwa mnaambiwa kuwa kwa Tanzania na Afrika Mashariki Timu Bora ni Simba SC pekee muache kuwa Wabishi na ndiyo maana hata kwa Afrika sasa ni ya Saba ( 7 ) kwa Viwango huku Wasiojua wengine pamoja na Kucheza Fainali ya CAFCC hata katika Top 20 tu hawapo.

Mkubwa ni Mkubwa tu Kudadadeki!!!!
Ngoja nikufukulie hili kaburi.
 
Tumsamehe mleta uzi, hii sio fani yake. Fani yake ni udaku, ushirikina, unafiki, uongo, na uchonganishi. Kwenye uelewa wa mpira, ufundi, mbinu na sheria za mpira ni mweupe kabisa yaani ni box.
 
Back
Top Bottom